Aliyekuwa kiongozi wa mungiki Maina ajisalimisha

Mnamo Mei 12, polisi pia walivamia nyumba zake Nairobi na Nyahururu wakisema walikuwa wakimtafuta.

Muhtasari
  • Njenga ametaja siasa mbaya katika madai ya hivi punde ya polisi.
  • Alisema hajawahi kumiliki bunduki wala kutumia bangi maishani mwake.
Maina Njenga
Maina Njenga
Image: STAR

Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga, Jumatano, Mei 24, alijisalimisha kwa mamlaka katika Mahakama ya Nakuru.

Wakili Ndegwa Njiru alimsindikiza Njenga hadi katika majengo ya mahakama, saa chache baada ya Kurugenzi ya Makosa ya Jinai kuanzisha msako wa kumtafuta.

Alikuwa na wakili wake Ndegwa Njiru alipojiwasilisha mahakamani.

Alikuwa amepata dhamana ya kutarajia Jumanne na kuwazuia polisi kumkamata au kumweka kizuizini kwa madai ya kupatikana na bunduki mbili na roli 90 za bangi.

Hapo awali, maafisa wa DCI walikuwa wakimsaka kuhusiana na kupatikana kwa bunduki mbili na zaidi ya roli 90 za bangi katika nyumba iliyohusishwa naye mjini Nakuru.

Njenga ametaja siasa mbaya katika madai ya hivi punde ya polisi.

Alisema hajawahi kumiliki bunduki wala kutumia bangi maishani mwake.

“Hii ni siasa. Polisi wanadanganya na hawafai kutumika katika michezo ya aina hiyo,” alisema.

Aliongeza kuwa hakuna mtu aliyewasiliana naye juu ya madai hayo.

“Rais hapaswi kuruhusu masuala hayo katika zama hizi. Ni siasa na hasa katika ukanda wetu,” aliongeza kwenye simu.

Polisi walisema wanamsaka Njenga kuhusiana na madai ya kupatikana kwa bunduki mbili na zaidi ya roli 90 za bangi kutoka kwa nyumba yake moja mjini Nakuru.

Njenga hakuwepo lakini polisi walipata wafanyikazi wanane humo wenye umri wa kati ya miaka 37 na 54 na kuongeza pia walipata risasi tatu tupu za 9mm zikiwa zimefichwa katika moja ya vyumba.

Moja ya bunduki zilizopatikana ni bastola ya kujitengenezea nyumbani inayoweza kufyatua huku nyingine ikiwa ni Tokarev ambayo nambari yake ya siri ilikuwa imeharibiwa, polisi walisema.

Mnamo Mei 12, polisi pia walivamia nyumba zake Nairobi na Nyahururu wakisema walikuwa wakimtafuta.

Njenga kisha akahusisha uvamizi huo na mazishi yaliyopangwa ya mke wa Dedan Kimathi, Field Marshal Mukami Kimathi mnamo Jumamosi, Mei 13, 2023, Njabini, Kinangop.

Njenga alisema timu hizo, ambazo zilifika sawia saa 4 asubuhi katika nyumba zake za Nakuru, Lavington, Karen na Nyandarua, ziliwaambia wafanyakazi kuwa walikuwa wakimtafuta.

Njenga alisema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kumzuia kuhudhuria mazishi.

 

 

 

 

 

 

 

Maina Njenga
Maina Njenga
Image: STAR