Kenya Kwanza yaiomba Azimio kurejelea mazungumzo

Murugara aliongeza kuwa atamwalika Amolllo kwa mazungumzo siku ya Jumatatu saa 2.30 usiku.

Muhtasari
  • Siku ya Alhamisi, Murugara alisema upande wa Kenya Kwanza umejitolea kuendelea na mazungumzo hayo.
  • Murugara hata hivyo alisema Kenya Kwanza haijakubali matakwa ya Azimio.

Kenya Kwanza imetaja uamuzi wa Azimio wa kusitisha mazungumzo ya pande mbili kama "mapema" ikisema hakukuwa na tofauti zisizoweza kusuluhishwa kati ya pande hizo mbili.

Akihutubia kikao na wanahabari katika Majumba ya Bunge Alhamisi, mwenyekiti mwenza wa kamati ya Kenya Kwanza George Murugara alisema Azimio haikumaliza njia zote za kusuluhisha tofauti ambazo huenda ziliibuka.

"Kuomba Kifungu cha 37 cha makubaliano kilikuwa mapema. Tunayo kifungu cha 34 kinachosema tukishindwa kufikia muafaka basi mwenyekiti mwenza wa pande hizo mbili akae na kujadili masuala hayo. Kifungu hiki kilirukwa,” alisema.

Murugara alisema upande wake utaangalia masuala yaliyoibuliwa na Azimio na kutoa majibu kwa mwenyekiti mwenza wa Azimio Otiende Amollo kufikia mwisho wa  siku ya Alhamisi.

Murugara aliongeza kuwa atamwalika Amolllo kwa mazungumzo siku ya Jumatatu saa 2.30 usiku.

Siku ya Jumatano, Azimio alitoa makataa ya siku sita kwa Muungano wa Rais William Ruto wa Kenya Kwanza kushughulikia wasiwasi wao ili mazungumzo yaendelee.

Makataa hayo yatakamilika Jumanne.

Azimio alisema wataona mazungumzo hayo yamevunjika na kuchukua hatua nyingine iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.

Siku ya Alhamisi, Murugara alisema upande wa Kenya Kwanza umejitolea kuendelea na mazungumzo hayo.

"Tuko tayari kuanza tena mazungumzo hata kesho," alisema huku akimsihi Azimio kutoweka "vizuizi visivyo vya lazima" wakati wa mazungumzo.

"Madai baada ya matakwa  kati si ya nia njema," aliongeza.

"Mwisho wa siku, ni matumaini yetu kwamba tutaanza mazungumzo," alisema.

Murugara hata hivyo alisema Kenya Kwanza haijakubali matakwa ya Azimio.

Azimio ameishutumu Kenya Kwanza ya upande wa Kenya Kwanza kwa kutokuwa na nia ya kushughulikia masuala muhimu; gharama ya maisha, ukaguzi wa seva za IEBC, urekebishaji na uundaji upya wa IEBC na mwisho wa kuchukua vyama tanzu vya Azimio.

 

 

 

Image: TWITTER