DP Gachagua awapa wanafunzi wa St Charles Lwanga Sh500,000 za 'lunch'

Gachagua pia aliahidi kuwanunulia wanafunzi basi la shule.

Muhtasari

•“Sasa mimi naona tufanye ile mambo ya chakula cha mchana, nitampa mkuu wa shule Sh500,000 kwa ajili ya chakula cha mchana,” Gachagua alisema.

•Gachagua pia alihoji ni kwa nini kiongozi wa Azimio Raila Odinga hakuhudhuria Harambee akisema Kitui ni ngome ya Raila.

akiwa na wanafunzi wa St Charles Lwanga katika Kaunti ya Kitui mnamo Juni 3, 2023
Naibu Rais Rigathi Gachagua akiwa na wanafunzi wa St Charles Lwanga katika Kaunti ya Kitui mnamo Juni 3, 2023
Image: DPCS

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa Sh500,000 kwa shule ya St Charles Lwanga, Kitui.

DP alikuwa ameenda shuleni humo kwa harambee kwa ajili ya maendeleo.

“Sasa mimi naona tufanye ile mambo ya chakula cha mchana, nitampa mkuu wa shule Sh500,000 kwa ajili ya chakula cha mchana,” alisema.

"Si mkikula chapati ni sawa, na soda."

Gachagua pia aliahidi kuwanunulia wanafunzi basi la shule.

“Mimi sijawahi sikia viongozi wenu wamenunua basi la shule, sasa naona Scania itaweza,” alisema.

Alisema ni muhimu kuweka fedha za kutosha katika shule hiyo ili kuimarisha maendeleo yake na kuwapa wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia.

"Sisi ni watu wa kazi, siasa imeisha tuko tayari kufanya kazi," alisema.

Gachagua pia alihoji ni kwa nini kiongozi wa Azimio Raila Odinga hakuhudhuria Harambee akisema Kitui ni ngome ya Raila.