Rais Ruto amteua mkuu mpya wa mkutano wa Africa Climate Summit

Bw. Ng’ang’a atafanya kazi kwa karibu na Waziri wa Mazingira Soipan Tuya na washikadau wengine.

Muhtasari
  • GEAPP iliundwa ili kusaidia kuharakisha nishati safi kwa kila mtu, kila mahali, kwa watu na sayari.
Rais Ruto amteua mkuu mpya wa mkutano wa Africa Climate Summit
Image: PCS

Rais William Ruto Ijumaa alimteua Joseph Ng’ang’a kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Mkutano wa Kilele wa Africa Climate Summit (ACS) utakaofanyika Septemba hapa Nairobi.

Bw. Ng’ang’a ni Makamu wa Rais wa Muungano wa Kimataifa wa Nishati kwa Watu na Sayari (GEAPP).

Ataongoza jopo la ACS na kusimamia upangaji na uratibu wa shughuli zote.

Bw. Ng’ang’a atafanya kazi kwa karibu na Waziri wa Mazingira Soipan Tuya na washikadau wengine.

GEAPP ni muungano wa hisani, serikali, teknolojia, sera na washirika wa ufadhili ulioanzishwa na The Rockefeller Foundation, IKEA Foundation, na Bezos Earth Fund.

GEAPP iliundwa ili kusaidia kuharakisha nishati safi kwa kila mtu, kila mahali, kwa watu na sayari.

Bw. Ng’ang’a pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafadhili wa Nishati Endelevu kwa Wote na mwanzilishi mwenza wa Africa Carbon Markets Initiative.

Mkutano wa kilele wa Afica Climate Summit utaandaliwa kwa pamoja na Kenya na Umoja wa Afrika mjini Nairobi kuanzia Septemba 4 hadi 6.

Bw Ng’ang’a alijiunga na Simon Harford, Mkurugenzi Mtendaji wa GEAPP, na William Asiko, Makamu wa Rais wa Rockefeller Foundation Africa, katika uzinduzi wake katika Ikulu ya Nairobi.