Ngunjiri Wambugu ajiunga tena na Jubilee saa chache baada ya Uhuru kuondolewa kama kiongozi wa chama

Wambugu alimtimua aliyekuwa Waziri Esther Murugi mnamo 2017 lakini akashindwa na Duncan Mathenge wa UDA

Muhtasari
  • Pamoja na Kanini na Sabina, Wambugu alipigia kampeni kiongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odingakuwa rais katika uchaguzi wa 2022.
Sabina Chege,aliyekuwa mbunge wa Nyeri na Kanini Kega
Image: KANINI KEGA/TWITTER

Aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu amejiunga tena na Chama cha Jubilee.

Wambugu, ambaye aliwahi kuwa mbunge kati ya 2017 na 2022, alikaribishwa kwenye Jubilee na Katibu Mkuu Kanini Kega na kiongozi wa chama Sabina Chege.

"Tunazidi kuimarika! Tulipokea Mh Ngunjiri Wambugu CBS aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini katika Jubilee NI Sisi!" Kanini alichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii siku ya Alhamisi.

Wambugu alimtimua aliyekuwa Waziri  Esther Murugi mnamo 2017 lakini akashindwa na Duncan Mathenge wa UDA ya Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu uliopita.

Pamoja na Kanini na Sabina, Wambugu alipigia kampeni kiongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odingakuwa rais katika uchaguzi wa 2022.

Aliyekuwa mbunge wa Nyeri Town alijiunga tena na Jubilee baada ya Msajili wa vyama vya kisiasa kuthibitisha kuwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amebadilishwa na Sabina kama Kiongozi wa Chama.

Katika notisi ya gazeti la serikali mnamo Jumatano, mbunge wa zamani wa Kieni Jeremiah Kioni alibadilishwa kama Sec General na Kanini huku Mbunge wa zamani wa Gatanga David Murathe akichukuliwa kama naibu mwenyekiti wa kitaifa na mbunge wa sasa wa Eldas Adan Keynan.