HALI YA UCHUMI

Maandamano kuendelea Jumatano, Alhamisi na Ijumaa - Azimio

Raia wametusihi kuendeleza maandamano hadi wasikizwe na Rais Ruto - Azimio la Umoja

Muhtasari

•Haya yanajiri wakati ambapo maandamano ya Jumatano 12 yaliacha watu 9 wakiaga dunia kwa mtutu wa bunduki.

Viongozi wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga.
Viongozi wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga.
Image: SCREENGRAB

Muungano wa Azimio la Umoja umetoa taarifa ukirekebisha kauli iliyotolewa Alhamisi 13, kuhusu kuandaa maandamano ya amani nchini kwa Wakenya ili kupinga gharama ya juu ya maisha.

Muungano huo katika taarifa yao umekiri kuwa ni kutokana na habari wanazotokea kutoka kwa Wakenya wakitaka maandamano hayo kuendelea hadi pale, serikali ya Kenya Kwanza itakaposikia matakwa yao.

Mawasiliano juu ya kauli iliyotolewa jana 13 kuhusu maandalizi ya wimbi la tatu la maandamano ya amani yaliyopangwa kuwa Jumatano wiki ijayo, kufuatia matakwa ya umma tunakiri kuwa muungano huu umerekebisha kalenda ya maandamno hayo. Kusonga mbele, maandamano hayo yataandaliwa Jumatano, Alhamisi na Ijumaa wiki ijayo, kutokana na matakwa ya raia. Tukutane Jumatano,” taarifa hiyo ilisema.

Image: Taarifa ya Azimio la Umoja

Maandamano ya Jumatano 12 yalikumbwa na ghasia nyingi zilizosababisha watu zaidi ya 10 kupoteza maisha yao huku mali ya kibinafsi na umma yakiharibiwa katika pilkapilka hizo za maandamano.

Wafanyibiashara bia walikadiria hasara kubwa siku hiyo, huku mduka ya jumla yakivunjwa na kuibiwa katika harakati hizo, huku baadhi ya watu pia wakikiri kuibiwa simu zai za mkononi katika harakati hizo.

Haya yanajiri wakati ambapo rais Ruto ameahidi kukabiliana vipasavyo na waandamanaji, huku akidai kuwa kile ambacho muungano wa Azimio la Umoja unatafuta ni “nusu mkate” ambapo alisema kuwa hilo halitawezekana katika serikali yake.

Rais alisema kuwa ameagiza serikali yake kukabiliana nao, kwani wanataka kuirudisha nchi nyuma, waaidha kiongozi wa Azimio anataka kuvuruga vijana kwa kuwa rais ana mpango wa kuwapa kazi.