NCIC yataka mazungumzo kati ya Ruto na Raila, inasema yametatizwa na mvutano uliokithiri

CIC imetaja mapigano yanayoendelea ya Sondu mpakani mwa Kericho-Kisumu kuwa huenda yamechochewa na mvutano baina serikali na upinzani.

Muhtasari

•NCIC imesema imeanzisha uchunguzi dhidi ya mapigano hayo ikisema kuwa yamechochewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa. 

Image: Wambui Nyutu naibu mwenyeki wa tume ya uiano

Rais William Ruto na kinara wa Upinzani Raila Odinga wamehimizwa kutafakari upya mazungumzo kama suluhu la wimbi la maandamano nchini. 

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano ilisema inasikitishwa na hali ya mvutano na maandamano ambayo ilibaini kuwa yamesababisha watu kupoteza maisha. Katika hotuba kwa wanahabari, makamu mwenyekiti wa Tume hiyo Wambui Nyutu alibainisha kuwa hali hii pia imebadilika na kuwa mizozo ya kikabila na ghasia. 

"Tunataka kuwaomba viongozi hao wawili kulegeza misimamo yao na kukumbatia mazungumzo ili kushughulikia masuala yanayoikumba nchi," alisema Nyutu. 

CIC imetaja mapigano yanayoendelea ya Sondu mpakani mwa Kericho-Kisumu kuwa huenda yamechochewa na mvutano baina serikali na upinzani. 

Hata hivyo, imesema imeanzisha uchunguzi dhidi ya mapigano hayo ikisema kuwa yamechochewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa. 

Nyutu alisema kwa sasa wanafanya kazi na afisi ya DCI huku watu wakitarajiwa kuanza wiki ijayo.