Viongozi wa Azimio wawatembelea wanafunzi waliorushiwa vitoa machozi

Rais William Ruto amekiri kwamba maandamano yanayopangwa na Azimio la Umoja Jumatano wiki ijayo hayatafanyika.

Muhtasari
  • Ziara yao inajiri siku mbili baada ya watoto hao kurushiwa gesi ya kuwatoa machozi wakati wa maandamano yaliyofanyika mnamo Jumatano wiki hii.
Viongozi wa Azimio wawatembelea wanafunzi waliorushiwa vitoa machozi
Image: EDWIN SIFUNA/TWITTER

Viongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya wakiongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Tim Wanyonyi (Westlands) na Babu Owino (Embakasi Mashariki), wamewatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kihumbuini.

Ziara yao inajiri siku mbili baada ya watoto hao kurushiwa gesi ya kuwatoa machozi wakati wa maandamano yaliyofanyika mnamo Jumatano wiki hii.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga aliitisha maandamano na kuwahimiza Wakenya wajitokeze kwa wingi kupinga hatua ya serikali ya Kenya Kwanza kuleta ushuru mpya ambao anasema utafanya gharama ya maisha kuendelea kupanda.

Hata hivyo muungano huo umeapa kuendelea na maandamano ya siku tatau wiki ijayo.

Muungano huo katika taarifa yao umekiri kuwa ni kutokana na habari wanazotokea kutoka kwa Wakenya wakitaka maandamano hayo kuendelea hadi pale, serikali ya Kenya Kwanza itakaposikia matakwa yao.

“Mawasiliano juu ya kauli iliyotolewa jana 13 kuhusu maandalizi ya wimbi la tatu la maandamano ya amani yaliyopangwa kuwa Jumatano wiki ijayo, kufuatia matakwa ya umma tunakiri kuwa muungano huu umerekebisha kalenda ya maandamno hayo. Kusonga mbele, maandamano hayo yataandaliwa Jumatano, Alhamisi na Ijumaa wiki ijayo, kutokana na matakwa ya raia. Tukutane Jumatano,” taarifa hiyo ilisema.

Rais William Ruto amekiri kwamba maandamano yanayopangwa na Azimio la Umoja Jumatano wiki ijayo hayatafanyika.

Ruto ameeleza kuwa ni kutokana na maandamano ya siku zilizopita ambapo watu waliaga dunia na wengine kupata majeraha mabaya huku mali yasiyokadirika yakiharibiwa na waandamanaji, ambapo alisema huwa hataruhusu hilo liendelee tena.

“Mliona juzi, walifanya maandamano Ijumaa iliyopita ile ingine watu saba wakakufa, wamefanya maandamano juzi watu nane wamekufa. Mimi nataka niwaulize, mnataka tuendelee na hii maandamano? Mnataka tuendelee na hii maandamano? Mimi nataka niwaambie, maandamano haiwezi kufanyika tena katika taifa la Kenya,” Aliuliza Ruto.