Watu 2 wajeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano Migori

Walilazwa katika hospitali ya makao ya wauguzi ya Oruba.

Muhtasari
  • Msimamizi wa hospitali hiyo Mike Ochere alithibitisha wanaume wawili wa umri wa makamo ambao walipata majeraha ya risasi walikuwa wakipokea matibabu katika kituo hicho cha afya.
Watu 2 wajeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano Migori
Image: SREENGRAB

Watu wawili wamepigwa risasi na kujeruhiwa na polisi katika maandamano ya kuipinga serikali yanayoendelea kaunti ya Migori.

Walilazwa katika hospitali ya makao ya wauguzi ya Oruba.

Msimamizi wa hospitali hiyo Mike Ochere alithibitisha wanaume wawili wa umri wa makamo ambao walipata majeraha ya risasi walikuwa wakipokea matibabu katika kituo hicho cha afya.

Mmoja wa wahasiriwa alipigwa risasi kwenye paja huku mwingine akipigwa risasi ya mguu.

Mwanamke wa umri wa makamo ambaye alikabiliwa na kukosa hewa baada ya polisi kufyatua vitoa machozi ndani ya nyumba yake alipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Polisi walisema wanachunguza tukio hilo.

Afisa mkuu alisema kumekuwa na makabiliano katika eneo hilo yaliyopelekea kupigwa risasi.

Hapo awali huduma za usafiri zililemazwa na biashara kufungwa ndani ya mji wa Migori kufuatia maandamano yanayoendelea Migori na miji mingine ndani ya Kaunti ya Migori.

 

Polisi wamewazuia waandamanaji hao kuingia katika eneo la biashara la Migori.

Waandamanaji hao walishirikiana na polisi katika kuendesha mapigano ndani ya mashamba yaliyo karibu na mji wa Migori.

Waandamanaji hao walishutumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa waandamanaji wa amani.

Maandamano hayo dhidi ya serikali yalifanyika katika maeneo tofauti nchini huku kukiwa na msako wa polisi dhidi ya viongozi hao.

Makumi ya viongozi walikamatwa katika operesheni ya polisi.

Vijana katika mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi wametoa wito na ombi kwa kinara wa Azimio Raila Odinga kusitisha maandamno ya sku tatu ambayo yameng’oa nanga mapema Jumatano.

Vijana hao wakiongozwa na kiongozi wa vijana KIbera Odhiambo Owino, walitoa wito kwa Odinga kusitisha maandamano hayo kwa kusema kwamba yatalemaza biashara zao.

Owino alisema kuwa gharama ya maisha kuwa juu si lawama kwa mtu yeyote hata serikali bali ni mfumko ambao umeshuhudiwa katika mataifa mengi duniani.

“Kwa siku ya leo unaona hivyo wamepanga ni maandamano ya siku tatu, lakini sisi wana Kibera ndio tunaumia san asana hii ghetto yetu. Sasa hivi hali ya uchumi iko juu na si eti ni lawama kwa mtu yeyote. Sasa hivi dunia yote kila kitu iko juu na si Kenya peke yake. Kwa hiyo hii mambo ya maandamano yanatuathiri hata Zaidi, yanaturudisha sifuri,” alisema Owino.