Uharibifu wa barabara Kisumu kugharimu Ksh.200M- CS Murkomen

Alitaja Kaunti ya Kisumu akisema barabara katika eneo hilo zimeharibika sana akisema serikali itatumia Ksh.200 milioni

Muhtasari
  • Matamshi yake yalizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku Wakenya wengi wakimkosoa kwa kuunda nambari hiyo wakitaka uthibitisho wa jinsi alivyofikia nambari hiyo ya kianga.
WAZIRI WA UCHUKUZI KIPCHUMBA MURKOMEN
Image: TWITTER

Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen sasa anasema kuwa uharibifu wa barabara katika mji wa Kisumu uliosababishwa na maandamano dhidi ya serikali utagharimu Ksh.200 milioni kukarabatiwa.

Murkomen, ambaye alizungumza Alhamisi katika Kaunti ya Isiolo, alikashifu upinzani akisema kuendelea kwa maandamano kutakuwa na pigo kwa nchi kifedha kutokana na uharibifu wa barabara na miundombinu mingine muhimu.

Alitaja Kaunti ya Kisumu akisema barabara katika eneo hilo zimeharibika sana akisema serikali itatumia Ksh.200 milioni kukarabati sehemu ndogo tu ya barabara katika Wilaya ya Biashara ya Kati jijini.

Nimegadhabishwa sana, ukiona tunatengeneza barabara kilomita moja tunatumia pesa kadri ya milioni 50 na 80. Alafu unaona mtu ambaye anasema nia yake ni gharama ya maisha ameenda kuweka matairi kwa barabara kuichoma,” he lamented.

”Kupitia pesa zao za taxes wanaambiwa baada ya mwaka tunafanya mainatinance na kesho tunatumia 50-80 million.”

Waziri huyo aliendelea: "Ukiona barabara zimechomwa Kisumu kwa wiki mbili zilizopita, tutahitaji si chini ya milioni 200 kwa eneo kidogo ya mji kuziba ile mashimo yameharibiwa kwa sababu mtu ameenda kuchoma matyres."

Murkomen alikariri kuwa uchomaji wa matairi huharibu lami nyingi na kusababisha mashimo.

Katika hali hiyo hiyo, Murkomen alitetea matamshi yake ya awali ambapo alisema uharibifu wa Barabara ya Nairobi Expressway wiki jana utailazimu serikali ya Ruto kukohoa Ksh.600 milioni kwa ukarabati.

Matamshi yake yalizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku Wakenya wengi wakimkosoa kwa kuunda nambari hiyo wakitaka uthibitisho wa jinsi alivyofikia nambari hiyo ya kianga.

Katika matamshi yake, hata hivyo, Murkomen alipuuzilia mbali wakosoaji akieleza kuwa akisisitiza kuwa barabara ni ghali kujenga na kudumisha akisema kwa sasa inagharimu kati ya Ksh.50 - Ksh.80 milioni kujenga kilomita moja ya barabara.

“Juzi niliambia wakenya kuwa tutalipa karibu nusu bilioni kulipia Expressway. Kuna wengine wanafanya mzaha hapo kwa mtandao kwa sababu hawaelewi,” alisema.