Chukuwa walinzi wangu ukitaka lakini nipe heshima - Uhuru kwa Ruto

Ukweli kwamba nimekuwa kimya haimaanishi kuwa naogopa. Kujeni kwangu," Uhuru alisema.

Muhtasari

• Uhuru alisema kuwa maafisa wa usalama wa mamake, mke wa rais wa kwanza wa taifa la Kenya Mama Ngina Kenyatta wameondolewa.

Image: Maktaba

Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amemjibu Rais William Ruto kuhusu hatua za hivi majuzi ambazo zimesababisha usalama rasmi wa familia yake kuondolewa.

Akizungumza Ijumaa usiku kufuatia madai ya polisi kuvamia nyumba ya mwanawe wa kwanza mtaani Karen, Uhuru aliitaka serikali ya Kenya Kwanza kuwachana na familia yake.

“Kama wanataka wachukue walinzi wangu lakini wanipe heshima yangu,” Uhuru alisema.

Uhuru aliendelea kusema kuwa katika siku chache zilizopita, maafisa wa usalama wa mamake, mke wa rais wa kwanza wa taifa la Kenya Mama Ngina Kenyatta wameondolewa, kitendo ambacho anakitaja kuwa cha kutiliwa shaka.

" Kuna waziri mzima wa serikali anasema atafanya nini, sijui mbele ya nyumba ya mama yangu. Watu ambao wamekuwa wakimlinda mama yangu kwa karibu miaka 50 iliyopita walitolewa usiku.

"Najiuliza serikali hii inataka nini? Ukweli kwamba nimekuwa kimya haimaanishi kuwa naogopa. Kujeni kwangu," Uhuru alisema.

Aliendelea kulaani tukio hilo akisema atachukua hatua za kisheria.

“Tukio hili nawaachia mawakili wangu,” alisema.