Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka azuiliwa nyumbani kwake, imedaiwa polisi wamezingira nyumba yake

Afisa wa mawasiliano wa Kalonzo Paloma Gatabaki alisema polisi wamekita kambi nje ya nyumba ya Kalonzo tangu siku ya Jumanne.

Muhtasari

• Kiongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga pia amethibitisha taarifa hizo akisema kuwa anasema kuwa Kalonzo Musyoka yuko kizuizini nyumbani kwake.

KALONZO MUSYOKA
Image: HISANI

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka sasa anadai kuwa amekuuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Jumanne.

Kulingana na  afisa wa mawasiliano wa Kalonzo Paloma Gatabaki, polisi wamekita kambi nje ya  nyumba yake tangu siku ya Jumanne.

Kiongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga pia amethibitisha taarifa hizo akisema kuwa anasema kuwa Kalonzo Musyoka yuko kizuizini nyumbani kwake.

Tangazo la Odinga kuhusu madai ya kuzuiliwa kwa Kalonzo linakuja baada ya ripoti kuibuka kuwa kiongozi huyo wa Chama cha Wiper alikuwa na mkutano wa faragha na kundi la wanadiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Denmark.

Sababu ya mkutano huo bado haijabainika. Hata hivyo, mkutano huo unajiri  wakati hali ya taharuki imetanda nchini kutokana na maandamano yalioyitishwa na muungano wa Azimio.

Viongozi wa Azimio-One Kenya
Image: EZEKIEL AMING'A

Raila ametetea kutokuwepo kwake katika maandamano ya siku tatu akisema anapumzika kutokana homa kali ambayo amekuwa akiugua.

"Sijafanya mkutano wowote na mabalozi kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari," Raila alisema.

Raila aliongeza kuwa...” "Nilipata homa mbaya sana... Lakini sasa nazidi kupata afueni. Nitakuwa sawa sawa.

Wakati wa maandamano ya siku tatu yaliyoitishwa na muungano wa Azimio viongozi wote wa muungano huo hawakujitokeza kushiriki bali waliachia wafuasi wao pekee kukabiliana na polisi.

Waandamanji kadhaa waliuawa  kwa kupigwa risasi huku wengine wengi wakikamatwa kwa madai ya kushiriki maandamano haramu na uharibifu wa mali.