Nitaendelea kumuunga mkono Raila licha ya vitisho - Uhuru

Siku ya Ijumaa, Uhuru alisema kuwa vitisho vyote kutoka kwa serikali havitamfanya akome kushirikiana na Raila.

Muhtasari

• Kulingana na Uhuru, Raila alikuwa na maono mazuri kwa nchi.

Kuvunjika kwa uhusiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na William Ruto kulitokana na makubaliano baina ya Kenyatta na Raila Odinga( kulia pichani) al maarufu 'Handshake'
Kuvunjika kwa uhusiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na William Ruto kulitokana na makubaliano baina ya Kenyatta na Raila Odinga( kulia pichani) al maarufu 'Handshake'
Image: BBC

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amesema uungwaji mkono wake kwa Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga hautabadilika.

Siku ya Ijumaa, Uhuru alisema kuwa vitisho vyote kutoka kwa serikali havitamfanya akome kushirikiana na Raila.

"Uungwaji mkono wangu bado uko kwa Raila. Ni rafiki yangu. Je, ni gaidi ambaye siwezi kuzungumza naye, hiyo ni haki yangu ya kidemokrasia. Katika katiba yetu, Wakenya walimpigia kura yeyote waliyemtaka,” Uhuru aliongeza.

Rais huyo wa zamani alisema alinyamaza na kukabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi kama ilivyotangazwa na IEBC.

"Nilimkabidhi na kuondoka," Uhuru alisema.

Uhuru alimuidhinisha mpinzani wake wa muda mrefu Raila Odinga kama mrithi wake aliyempendelea katika uchaguzi wa Agosti 2022.

Kulingana na Uhuru, Raila alikuwa na maono mazuri kwa nchi.

Ruto ambaye wakati huo alikuwa naibu wa Uhuru hata hivyo alimshinda Raila katika uchaguzi wa urais na kuapishwa rais wa tano wa Kenya.

Ruto alipata kura milioni 7.1 dhidi ya kura milioni 6.9 za Raila.. Ushindi wa Ruto hata hivyo hautambuliwa na upinzani.