Madaktari wa KNH wafanikiwa kukiongezea damu kijusi ndani ya tumbo la uzazi la mama yake

Madaktari hao ni pamoja na Rosa Chemwey, Flavia Ogutu, Ikol Adung'o na Kunjira Murayi,

Muhtasari
  • Utaratibu huo wa umakini zaidi, unaojulikana kama Uhamisho wa Ndani wa Kijusi ni hatua muhimu katika matibabu ya kijusi na utaalamu wa tiba ya ndani ya mwili wa mama.

Madaktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta wamefanikiwa kutia damu kwa kijusi akiwa bado kwenye mfuko wa uzazi wa mama huyo.

Kupitia taarifa kwa vyumba vya habari, hospitali kubwa zaidi ya rufaa nchini ilisema kuwa utaratibu huo nyeti sana, unaojulikana kama utiaji mishipani wa kijusi, unahusisha kudungwa kwa chembechembe nyekundu za damu kutoka kwa wafadhili hadi kwa kijusi.

Utaratibu huo wa umakini zaidi, unaojulikana kama Uhamisho wa Ndani wa Kijusi ni hatua muhimu katika matibabu ya kijusi na utaalamu wa tiba ya ndani ya mwili wa mama.

Timu ya madaktari bingwa wanne walifanya utaratibu huo wa kimatibabu ambapo chembe nyekundu za damu kutoka kwa wafadhili hudungwa ndani ya kijusi.

Uhamisho wa ndani ya mfuko wa uzazi unaweza kupendekezwa wakati kijusi kina upungufu wa damu au Anemia (hali inayopunguza seli za damu).

Madaktari hao ni pamoja na Rosa Chemwey, Flavia Ogutu, Ikol Adung'o na Kunjira Murayi, Mtaalamu wa tiba ya miale.

Walisaidiwa na Benson Nyankuru na Redempata Mumo ambao ni wauguzi, na Tony Wainaina, Afisa wa Kliniki ya Afya ya Uzazi.

Kwa kutumia kipimo cha ultrasound ili kubainisha nafasi ya kijusi na na kondo la nyuma la uzazi, daktari wa upasuaji huingiza sindano kwenye fumbatio la mama na kisha kwenye mshipa wa kitovu cha kijusi.