Msichana jasiri asifiwa kwa kukabiliana na viongozi wa Uasin Gishu ana kwa ana kuhusiana na sakata ya Finland

Msichana huyo alilalamika kuhusu kuchelewa kwa viongozi kwenye mkutano huo na kudai suluhu la pesa zao zilizotoweka.

Muhtasari

•Mhitimu huyo alidokeza kuwa licha ya kumaliza shahada yake ya chuo kikuu, sasa amelazimika kuuza uji ili kujikimu kimaisha.

•"Unatabasamu kwa ulimi laini sana na uso laini unaoonekana hauna hatia lakini unaendelea kusema uwongo na uwongo!”” msichana huyo alimlalamikia naibu gavana.

akiwasuta hadharani viongozi wa Uasin Gishu.
Mhitimu wa Kabarak University akiwasuta hadharani viongozi wa Uasin Gishu.
Image: HISANI

Msichana mmoja mwenye umri wa ujana kutoka Uasin Gishu amegeuka kuwa gumzo mitandaoni baada ya video yake akiwasuta viongozi wa kaunti hiyo kuhusiana na mradi wa elimu wa Finland kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kabarak ambaye alikuwa amehudhuria mkutano kati ya viongozi, wazazi na baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na mradi huo wa elimu uliofeli mwanzo aliwakosoa viongozi hao kwa kuchelewa kufika kwenye mkutano huo.  Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim, Naibu Gavana John Barorot na seneta Jackson Mandago.

Msichana huyo kisha alibainisha jinsi watoto wa viongozi hao walivyosoma katika vyuo vikuu vya kifahari huku wengine wakipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya masomo ilhali watoto wa watu wasio na utajiri mkubwa ambao wazazi wao walijitolea kupata pesa za kuwapeleka nje ya nchi kwa ajili ya elimu wamefikia kukumbwa na msongo wa mawazo baada ya pesa zao kutoweka kwa njia isiyoeleweka.

“Kuna wanafunzi hapa wanatumia dawa za kupunguza msongo wa mawazo. Nilimaliza shule 2021, nilihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kabarak. Binti yako alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Riara, labda haikusumbui. Niliona na nikampongeza. Nilimuuliza nini kinafuata, akaniambia hajui, ataniambia. Baada ya hapo hatukuzungumza. Sasa, umempa mwanzo wa miezi kadhaa,” msichana huyo alilalamika.

Mhitimu huyo alidokeza kuwa licha ya kumaliza shahada yake ya chuo kikuu, sasa amelazimika kuuza uji ili kujikimu kimaisha.

“Hatukuwapa kibali cha kutumia pesa zetu kuwalipia wanafunzi wengine. Hatutaki kusikia hadithi nyingi. Bw Barorot kwa hakika Bw Chepses alisema ukweli, wewe ni mbaya sana na ukweli, mbaya sana. Utatudanganya siku kwa siku. Sijui kama umetumwa na wakuu wako. Kwa hakika sina cha kuishi kwa ajili yake, kwahiyo unaweza kutuma tu wahuni wako wakienda kuniua, ni sawa angalau sitakuwa nimejiua," alisema.

Aliongeza, "Nitakuambia ukweli, wewe ni mbaya sana na ukweli. Unaendelea kusema uwongo, unatutabasamu kwa ulimi laini sana na uso laini unaoonekana kuwa hauna hatia lakini unaendelea kusema uwongo na uwongo!”

Wakenya wanaotumia mitandao wamestaajabishwa na kuvutiwa na ujasiri wa msichana huyo na hivyo kumpongeza kwa kusimama bila kutikiswa.

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa baadhi ya Wakenya;

ericomondi: Namtafuta Msichana huyu kwa Haraka!!! Yeyote mwenye Mawasiliano yake tafadhali DM🙏🙏. WAKATI WETU NI SASA!!! Hakuna atakayetuokoa,..

Cornelius K. Ronoh: This Uasin Gishu girl is breathing fire. She has lectured Mandago like a baby.

Eng. Nyasikera: This girl addressing Mandago, Barorot and Chelilim on the Finland scam is the reason Gen Z make me happy. They have no chills. I would want my children to question anything that doesn't feel right. She is very respectful too.

Abuga Makori EGH, MBE: We need such BOLD and COURAGEOUS young people. This girl had guts to lecture likes of Jackson Mandago and Uasin Gishu politicians over fraudulent Finland "air lift programme". President William Ruto should reprimand these thieves led by Mandago, compel them to refund poor parents.

khalif kairo: That girl from Uasin Gishu who confronted Mandago is my hero. This leaders are our parents and we respect them,lakini they should know unlike them we are smarter we have the internet and we won’t take shit from them.