Mwanamke ajisalimisha kwa kumuua mpenziwe kwa kumduga kisu

Mwanaume kufariki baada ya kudugwa kisu na mpenzi wake wa baa

Muhtasari

• Polisi kujunguza kifo cha mwanamke aliyemduga mpenzi wake na kujisalimisha

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Mwanamke mmoja amejisalimisha kwa polisi baada ya kumuua mpenzi wake kwa kumdunga kisu katika kaunti ya Kirinyaga.

Hofu  imetanda katika  kituo cha kibiashara cha Kagio kaunti ya Kirinyaga baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 38 kumuua mpenziwe kwa kumdunga kisu mara tano.

Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kirinyaga Magharibi Moses Koskei, mwanamke huyo ambaye ni mhudumu wa baa katika kituo hicho cha biashara alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Kagio siku ya Jumatatu baada ya kisa hicho.

“Alimdunga kisu mpenzi wake mara tano; mara mbili kwenye paja la kushoto, mara mbili kwenye paja lake la kulia na mara ya tano katika sehemu zake za siri,” Koskei alisema.

Koskei alisema mwanamume huyo alifariki baada ya kuvuja damu na polisi wanachunguza sababu ya mwanamke huyo alimuua mpenzi wake.

"Wawili hao wamekodisha nyumba kando ya Barabara ya Baricho katika kituo hiki cha kibiashara na tunaambiwa wote wanatoka eneo bunge la Gichugu," Koskei alisema.

Mkuu wa polisi alisema bado hawajapata kisu cha muuaji.

"Tunamtarajia mshukiwa ambaye anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kagio atuambie alificha wapi silaha ambayo tutaitumia kama ushahidi," Koskei alisema.

Mwili wa mhasiriwa ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Kerugoya.