Nairobi Hospital yaomboleza kifo cha mkurugenzi wa fedha Erick Maigo

Maigo, 40, alipatikana Ijumaa asubuhi akiwa ameuawa katika nyumba yake eneo la Woodley, Nairobi.

Muhtasari
  • Mshambulizi wake, mwanamke ambaye pengine alikuwa amekesha usiku kwenye nyumba hiyo au aliifikia asubuhi alitoroka dakika chache kabla ya polisi kufika.

Nairobi hospital mnamo Ijumaa iliomboleza mkurugenzi wa fedha wa hospitali hiyo Erick Maigo.

Maigo, 40, alipatikana Ijumaa asubuhi akiwa ameuawa katika nyumba yake eneo la Woodley, Nairobi.

Katika taarifa yake, Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Nairobi James Nyamongo aliwaomba wahudumu wa Hospitali hiyo watulie wanapokabiliana na hali hiyo ya kusikitisha.

“Taarifa ambazo hazijathibitishwa tunazo kwa sasa kwamba mwili wa Eric ulipatikana nyumbani kwake na majirani asubuhi ya leo mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi,” alisema.

"Eric alikuwa mfanyakazi aliyejitolea sana ambaye alijitolea kwa uwezo wake wote kwa ufanisi wa The Nairobi Hospital. Hebu sote tuweke familia yake katika maombi yetu wanapopitia wakati huu wa majaribu."

Kulingana na hospitali hiyo, familia yake ilikuwa imefahamishwa kuhusu tukio hilo la kusikitisha.

Mshambulizi wake, mwanamke ambaye pengine alikuwa amekesha usiku kwenye nyumba hiyo au aliifikia asubuhi alitoroka dakika chache kabla ya polisi kufika.

Mkuu wa polisi wa Kilimani, Moss Ndiwa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo, akisema wapelelezi wanamsaka mshukiwa

Polisi walisema mwili huo ulikuwa na majeraha 16 ya kuchomwa visu.

Majeraha kumi kati ya hayo yalikuwa kifuani na upande wa nyuma. Haijulikani ikiwa mwanamke huyo alitenda peke yake