Maafisa wa KDF waaga dunia baada ya ajali ya Helikopta Lamu

KDF ilibaini katika taarifa hiyo bodi ya uchunguzi imeundwa na kutumwa katika eneo la tukio ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Muhtasari
  • Katika taarifa, KDF ilitaja ndege iliyoanguka kama Helikopta ya Huey lakini haikufichua idadi ya wanajeshi waliokuwemo wakati ilipoanguka.

Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jumanne lilitangaza kwamba helikopta yake ya uchunguzi ilianguka katika Msitu wa Boni, Kaunti ya Lamu Jumatatu usiku wakati wa doria ya kawaida.

Katika taarifa, KDF ilitaja ndege iliyoanguka kama Helikopta ya Huey lakini haikufichua idadi ya wanajeshi waliokuwemo wakati ilipoanguka.

KDF imeendeleza zoezi la uokoaji huku uchunguzi kuhusu ajali hiyo ukianza.

Hii ni ajali ya pili mwaka huu, hata wataalamu wakihoji kustahiki kwa ndege za kijeshi za Kenya.

"Helikopta ya Kenya Air Force Huey ilipondwa jana usiku ilipokuwa doria usiku katika Kaunti ya Lamu. Wafanyakazi na wanajeshi wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa sehemu ya kikosi cha anga kilichoimarisha doria za mchana na usiku na ufuatiliaji wa Operesheni inayoendelea Amani Boni," KDF ilisema. 

KDF ilibaini katika taarifa hiyo bodi ya uchunguzi imeundwa na kutumwa katika eneo la tukio ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Helikopta ya Huey ni helikopta ya matumizi ya kijeshi iliyoundwa na kuzalishwa na kampuni ya anga ya Amerika ya Bell Helicopter.