Kirinyaga: Mwanamke apatikana amefariki bafuni

Kulingana na walioshuhudia walisema mwanamke huyo alitumia Jumapili nzima kufagia nyumba yake.

Muhtasari

• Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana na mpangaji mwingine ambaye alikuwa ameingia bafuni.

• Mwanafamilia anayeitwa Joy Wangari alifichua kwamba mwanamke huyo alikuwa tu katika nyumba ya kukodi kwa wiki mbili.

polisi wachunguza kifo cha mwanamke Kirinyanga
polisi wachunguza kifo cha mwanamke Kirinyanga

Hali ya simanzi ilitanda baada ya wakaazi wa ploti moja katika mji wa Kagio, Kaunti ya Kirinyaga baada ya maiti ya mwanamke mwenye umri wa miaka 40 kugunduliwa bafuni Jumapili usiku.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana na mpangaji mwingine ambaye alikuwa ameingia bafuni.

Kulingana na  walioshuhudia walisema mwanamke huyo alitumia Jumapili nzima kufagia nyumba yake.

Mwanafamilia anayeitwa Joy Wangari alifichua kwamba mwanamke huyo, mama wa watoto wawili, alikuwa tu katika nyumba ya kukodi kwa wiki mbili.

Aliongeza kuwa marehemu alikuwa amehama kutoka Nairobi na mumewe. Mimi ndiye niliyewashauri kukodi nyumba huko Kagio baada ya gharama ya juu ya maisha Nairobi.

"Yeye ni mama wa watoto wawili na amekaa hapa kwa wiki moja tu na mumewe anakuja sasa hivi kutoka Nairobi,” Wangari alisema kama ilivyoripotiwa na wanahabari Wangari alionyesha mshtuko wake mkubwa katika mabadiliko hayo ya kusikitisha.

Polisi katika kaunti ndogo ya Mwea-magharibi wanachunguza chanzo cha kifo cha mwanamke huyo.

"Tutajua sababu ya kifo chake baada ya uchunguzi wa maiti." Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochwari ya Kibugi ukisubiri uchunguzi wa kifo chake.