Mwanamume ashtakiwa kwa kuwapiga watoto wake watatu hadi kufa

Na mke wake wa zamani ameshtakiwa kwa vifo vya wavulana hao wawili.

Muhtasari
  • Polisi wanaamini kwamba wengine wawili huenda walizikwa chini ya eneo ambalo sasa kipo kituo cha mafuta.
Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Polisi nchini Thailand wamemshtaki mwanamume mmoja kwa kumpiga hadi kumuua bintiye wa miaka miwili na wanawe wawili wachanga wakiume.

Wanashuku kuwa Songsak Songsaeng pia aliwaua watoto wengine wawili wa kiume kutoka kwa ndoa yao ya awali.

Mashtaka hayo yanafuatia kugunduliwa wiki iliyopita kwa mwili wa msichana wa miaka miwili uliozikwa chini ya sakafu ya jikoni.

Polisi wanasema Bw Songsak anadai kuwa na historia ya ugonjwa wa akili - na kwamba aliwaua watoto wake kwa sababu hakuweza kuvumilia sauti ya kilio chao.

Mkewe pia ameshtakiwa kwa kifo cha binti yao wa miaka miwili.

Na mke wake wa zamani ameshtakiwa kwa vifo vya wavulana hao wawili.

Wote watatu wamekamatwa. Bw Songsak ameoa mara nne.

Polisi walitahadharishwa kwa mara ya kwanza kuhusu uwezekano wa kisa cha unyanyasaji wa nyumbani katika wilaya ya Bang Khen mjini Bangkok mapema mwezi huu.

Majirani wa Bw Songsak waliripoti kuwa binti zake wawili, wenye umri wa miaka 12 na minne, walikuwa wakidhulumiwa kimwili.

Polisi waliwaokoa binti hao wawili walipokuwa nyumbani peke yao.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 aliwaambia polisi kwamba wazazi wao walimpiga dadake mwenye umri wa miaka miwili, jambo ambalo lilisababisha kifo chake.

Pia alisaidia polisi kufuatilia mwili huo hadi ulipozikwa chini ya sakafu ya jikoni kaskazini-magharibi mwa Thailand wiki iliyopita.

Polisi wa Thailand pia wamemshtaki Bw Songsak kwa mauaji ya wana wengine wawili wa kiume aliokuwa nao na mke wake wa tatu baada ya DNA yake kufanana na ya watoto wawili wachanga, ambao miili yao ilifukuliwa miaka 10 iliyopita.

Mkewe wa tatu alisema kuwa aliwaua wana wao wachanga wanne na kuwaonyesha polisi mahali ambapo wawili walizikwa.

Polisi wanaamini kwamba wengine wawili huenda walizikwa chini ya eneo ambalo sasa kipo kituo cha mafuta.