EACC yatoa onyo kali dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za El Nino

Pesa nyingi zimepangwa kutolewa kwa Kaunti za Ardhi Kame na Nusu Kame (ASAL) ambazo zinakadiriwa kukumbwa na mvua hiyo.

Muhtasari
  • Kwa hivyo Bw. Mbarak alisema kuwa taasisi yoyote iliyopewa mamlaka ya kupunguza athari za El Nino inapaswa kufanya kazi ndani ya mipaka ya sheria,
Afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak.
Afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak.

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imetoa onyo kali kwa watu wanaonuia kufuja pesa za umma katika hatua zinazoendelea za kukabiliana na athari za mvua za El Nino.

Mkurugenzi Mtendaji wa tume Twalib Mbarak, katika taarifa kwa vyumba vya habari, alisema wana habari kwamba kuna kupuuzwa kwa sheria katika kuanzishwa kwa hatua hizo, ambazo huenda zikachochea udanganyifu katika serikali za kaunti na kitaifa.

Kwa hivyo Bw. Mbarak alisema kuwa taasisi yoyote iliyopewa mamlaka ya kupunguza athari za El Nino inapaswa kufanya kazi ndani ya mipaka ya sheria, na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote atakayepatikana na hatia.

"Tume inashauri kwamba ununuzi na matumizi yote yanayofanywa na Wizara/Idara na Wakala za Serikali ya Kitaifa (MDAs) na serikali za Kaunti katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, katika maandalizi ya mvua zinazotarajiwa za El Nino zinapaswa kuzingatia kikamilifu sheria za ununuzi, Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma, na. kanuni,” alisema.

"Maafisa wa hesabu watawajibishwa kibinafsi kwa hasara yoyote, matumizi yasiyoidhinishwa, au matumizi mabaya ya fedha za umma."

Serikali inasema inapanga kutenga kiasi cha Ksh.10 bilioni ili kudhibiti athari za mvua za El Nino zinazotarajiwa kuanza katikati ya Oktoba na kuendelea hadi mwisho wa Desemba.

Pesa nyingi zimepangwa kutolewa kwa Kaunti za Ardhi Kame na Nusu Kame (ASAL) ambazo zinakadiriwa kukumbwa na mvua hiyo.