Kila mwanachama wa Hamas ni mfu, Netanyahu anasema

Akiwa pamoja na Netanyahu, kiongozi wa upinzani Benny Gantz alisema pia kwamba Israeli ipo katika "wakati wa vita".

Muhtasari

• Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa amezungumza na Bw Netanyahu na kuweka wazi kwamba Israel lazima "ifanye kazi kwa kuzingatia sheria za vita".

• Bw Biden alisema anaelewa hasira na kufadhaika kwa watu wa Israel lakini akahimiza Israel kuzingatia kanuni za mikataba ya Geneva.

ni miongoni mwa wanachama wa "baraza la mawaziri la vita" la muda
Benjamin Netanyahu (kushoto) na Benny Gantz (kulia) ni miongoni mwa wanachama wa "baraza la mawaziri la vita" la muda
Image: REUTERS/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCKC

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kila mwanachama wa Hamas ni "maiti" baada ya mkutano wa kwanza wa serikali ya dharura ya nchi yake.

Akiwa pamoja na Netanyahu, kiongozi wa upinzani Benny Gantz alisema pia kwamba Israeli ipo katika "wakati wa vita".

Lakini Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa amezungumza na Bw Netanyahu na kuweka wazi kwamba Israel lazima "ifanye kazi kwa kuzingatia sheria za vita".

Idadi ya vifo nchini Israel imefikia 1,200. Zaidi ya watu 1,100 wameuawa kwa mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza.

Bw Biden alisema anaelewa hasira na kufadhaika kwa watu wa Israel lakini akahimiza Israel kuzingatia kanuni za mikataba ya Geneva.

Pia aliionya Iran - ambayo imeafiki shambulio la Hamas - "kuwa makini".

Mapema Jumatano Bw Netanyahu na Bw Gantz walikubaliana kuweka kando uhasama wao mkali wa kisiasa ambao ulikuwa umeongezeka na kusababisha maandamano makubwa.

Bw Gantz aliwaambia raia wa Israel kwamba serikali mpya iliyoundwa "imeungana" na iko tayari "kufuta kitu hiki kinachoitwa Hamas kutoka kwenye uso wa dunia".

Pamoja na Bw Netanyahu na Bw Gantz, kiongozi wa chama cha National Unity Party na waziri wa zamani wa ulinzi, baraza jipya la mawaziri la muda pia litajumuisha Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Yair Lapid, hajajiunga na muungano huo. Hata hivyo, Bw Netanyahu na Bw Gantz walisema katika taarifa ya pamoja kwamba k atatengewe kiti katika baraza la mawaziri la vita.