Katibu wa Kudumu Susan Mang’eni ahusika kwenye ajali, mmoja akifariki

Polisi walisema mwendesha pikipiki huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofika hospitalini.

Muhtasari

• Polisi walisema mwendesha pikipiki huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofika hospitalini.

Image: alilmokuwa akisafiria katibu mkee wa Susan Mange'ninn

Mwendesha pikipiki mmoja alifariki papo hapo baada ya pikipiki yake kugongana ana kwa ana na gari la Katibu wa kudumu Biashara ndogo za kadri na ndogo Susan Mang’eni.

Ajali hiyo ilitokea Oktoba 16 katika eneo la Korinda, Kaunti ya Busia. Polisi walisema mwendesha pikipiki huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofika hospitalini.

Katibu wa kudumu wa SME Susan Mang'eni akipokea matibabu baada ya kuhusika katika ajili ya barabarani Busia.
Katibu wa kudumu wa SME Susan Mang'eni akipokea matibabu baada ya kuhusika katika ajili ya barabarani Busia.
Image: HISANI

 Kulingana na polisi Mange’eni na dereva wake pia walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini. Polisi hata hivyo walithibitisha kuwa Mang’eni hakuwa katika hali ya hatari na kwamba anaendelea kupata nafuu. Polisi walisema kilichosababisha ajali hiyo. Amelazwa katika hospitali ya Busia.

Gari la serikali alilokuwa akiisafiriwa Mang’eni liliharibika vibaya na kubururwa hadi kituo cha polisi karibu na eneo la ajali.