Afueni kwa vyuo vikuu, serikali yatangaza kutolewa kwa ufadhili wa elimu

Machagu alisema kuwa fedha hizo zitapelekwa kwenye vyuo vikuu na akaunti za wanafunzi kuanzia Jumanne tarehe 7 Novemba 2023.

Muhtasari

• Waziri wa Elimu Ezekiel Machagu alisema kuwa fedha hizo zitapelekwa kwenye vyuo vikuu na akaunti za wanafunzi kuanzia Jumanne tarehe 7 Novemba 2023.

 

WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU
Image: ANDREW KASUKU

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imekamilisha mchakato wa kutoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika vyuo vikuu na taasisi za TVET chini ya Mfumo Mpya wa Ufadhili wa Elimu ya Juu.

“Hivyo basi, Wizara inapenda kuwafahamisha waombaji waliofaulu kuwa fedha hizo zitapelekwa kwenye vyuo vikuu na akaunti za wanafunzi kuanzia Jumanne tarehe 7 Novemba 2023”, ilisomeka notisi ya waziri wa elimu Ezekiel Machogu.

Serikali ilibadili mfumo wa ufadhili wa elimu katika vyuo vikuu na taasisi za TVET kuanzia mwaka huu. Hatua hiyo hata hivyo ilikuwa imezua tumbo joto miongoni mwa wanafunzi na vyuo kwa sababu tangu wanafunzi wajiunge na vyuo vikuu serikali ilikwa haijawasilisha pesa kwa vyuo vikuu.

Kabla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunga na taasisi za kulikuwa na hali ya swintofahamu kuhusu mfumo mpya wa ufadhili, hali iliyokuwa imewaacha wazazi katika njia panda, hata hivyo serikali iliagiza vyuo vyote vikuu vya umma kuwaruhusu wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza kuanza masomo huku serikali ikitathmini maombi ya wanafunzi.

Tangazo la waziri Machogu la kutolewa kwa pesa za mkopo ni afueni kwa vyuo vikuu ambavyo vilikuwa vinakumbwa na changamoto za kifedha.