Kalonzo: Mimi ndiye mgombeaji bora zaidi kumshinda Ruto 2027

Alisema kinara wa ODM Raila Odinga amedokeza kwamba ataunga mkono azimio lake.

Muhtasari

•Kalonzo alisema ana imani kwamba akiungwa mkono na wakuu wengine wa Azimio, ataibuka mshindi na kuwa rais wa sita.

•Alisema Raila alikuwa amedokeza kwamba wakati huu atahamasiha wafuasi wake kumuunga mkono kuwania kiti cha Urais.

KALONZO MUSYOKA
Image: HISANI

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ametangaza kuwa atasimama kama mgombeaji urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Kalonzo alisema ana imani kwamba akiungwa mkono na wakuu wengine wa Azimio, ataibuka mshindi na kuwa rais wa sita.

Alisema kinara wa ODM Raila Odinga amedokeza kwamba ataunga mkono azimio lake wakati huu kama mpeperushaji bendera wa Muungano huo akiwa amemuunga mkono mara tatu mfululizo.

“Raila hana budi kuniunga mkono wakati huu. Wakati wa kura za 2022, uliniambia nijiandae peke yangu. Viongozi walikuja na kuniambia niunge mkono ombi la Raila karibu na wiki moja ya kupiga kura na nilifanya hivyo na bado tuko pamoja,” Kalonzo alisema.

Makamu huyo wa Rais wa zamani alizungumza wakati wa kuchangisha pesa katika kanisa katoliki la Kyua katika eneo la Yatta, Kaunti ya Machakos Jumamosi.

Alisema Raila alikuwa amedokeza kwamba wakati huu atahamasiha wafuasi wake kumuunga mkono kuwania kiti cha Urais.

"Ndugu yetu (Raila) alisema mawazo yake na bado tunatembea pamoja na haturudi nyuma," Kalonzo alisema.

Kalonzo alisema Wiper Democratic Alliance imezindua zoezi la kitaifa la kusajili wanachama ili kuimarisha chama kwa idadi kabla ya uchaguzi ujao.

Hii alisema ni moja ya maandalizi ya kuunganisha msingi wa kugombea urais kitaifa.

"Kuna roho mpya kutoka kwa Kyua leo, ninyi ndio wengi. Serikali za kaunti za Machakos, Makueni na Kitui ni za Wiper Democratic Movements zilizo na Magavana na Maspika. Mnahitaji kusonga kwa kasi ili mwanzo wa Mwaka Mpya wa 2024 kwa neema ya Mungu, muanze kusajili wanachama wa Wiper ili kuhakikisha kuwa wote wanajiunga na chama," Kalonzo aliambia wanasiasa wa Wiper.

“Roho ya kujiunga na Wiper ni jinsi nilivyoona hapa leo. Ukipata kusajili wanachama katika Kenya ya eneo la Kati, Bonde la Ufa, Magharibi, na Nyanza miongoni mwa maeneo mengine, tutafanya hili kuwa vuguvugu la kweli la mabadiliko ya kweli katika nchi hii. Tuko tayari,” Kalonzo alisema.