Cherargei atimuliwa Kwenye kikao cha Seneti wakati wa kumhoji CS Murkomen

Hivi majuzi Cherargei ameonekana akimashambulia waziri Murkomen kwa maneno, kiasi cha kumtaka Rais William Ruto amwachishe kazi.

Muhtasari

• Cherargei alipuuza uamuzi wa spika na kuendelea kusimam kinyume na sheria za bunge hilo huku Waziri Murkomen akiendelea kuzungumza. 

• Cherargei alipuuza uamuzi wa spika na kuendelea kusimam kinyume na sheria za bunge hilo huku Waziri Murkomen akiendelea kuzungumza. 

Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Image: STAR

Seneta wa Nandi Samson Cherargei Jumatano alifukuzwa nje ya Seneti wakati wa hafla ya Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen.

Katika video za  kikao hicho unamwonyesha Murkomen akijibu swali kuhusu fidia ya maskwota anaposimama na kisha spika, Seneta Abdulkadir Haji, akimtaka Cherargei kumpa Waziri huyo nafasi ya kujibu maswali yote.

Cherargei alipuuza uamuzi wa spika na kuendelea kusimam kinyume na sheria za bunge hilo huku Waziri Murkomen akiendelea kuzungumza. 

Spika alilazimika  kukabili hali hiyo kwa mujibu wa sheria zinazo ongoza vikao vya bunge na kukatiza maelezo ya waziri Murkomen ya hali ya ujenzi wa Barabara ya Tala-Oldonyo Sabuk.

"Kwa wakati huu,umepatikana inje ya kanuni," Haji anamwambia Cherargei, ambaye anaonekana akimfokea Waziri Murkomen.

"Haya si mazishi," Haji alisisitiza.

Spika alimtaka Cherargei atoke nje ya Bunge ili kikao kiendelee kadri kilipokuwa kimeshuhudiwa,huku akijaribu kudinda lakini anaongozwa na seneta wa Busia Okiya Omtatah, mwenzake wa Kakamega Boni Khalwale na sajenti wawili wa bunge hilo.

Hivi majuzi Cherargei ameonekana akimashambulia waziri Murkomen kwa maneno, kiasi cha kumtaka Rais William Ruto amwachishe kazi.

Mnamo Novemba 8, alirushe cheche za maneno kwa Murkomen  akisema "Anachukua kipaza sauti na wakorofi, anawatukana na kuwadhalilisha watu na viongozi waliochaguliwa hata kwenye mazishi! Mamlaka ya uteuzi lazima itawale kwa Makatibu hawa wabaya wa baraza la mawaziri."