Mafuriko ya Manyara: Idadi ya watu waliofariki yafikia watu 80

Rais Samia Suluhu alisema serikali imepata maeneo ya kuwahamishia waathirika wa janga la mafuriko na maporomoko.

Muhtasari

• Waliojeruhiwa wamekuwa wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa hali zao zinapokuwa zimeimarika.

Image: Ikulu Tanzania

Msemaji wa serikali ya Tanzania amesema Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na janga la mafuriko na maporomoko ya udongo wilayani Hanang kaskazini mwa nchi hiyo imefikia watu 80.

Watu wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa katika janga hilo.

Alhamisi Rais wa Tanzania Samia Suluhu alisema serikali imepata maeneo ya kuwahamishia waathirika wa janga la mafuriko na maporomoko ya udongo wilayani Hanang kaskazini mwa nchi hiyo na itahakikisha hilo linafanyika kwa haraka.

Rais Samia alipokuwa akiwa na manusura wa janga la Hanang alipowazuru Alhamisi kuwajulia hali
Rais Samia alipokuwa akiwa na manusura wa janga la Hanang alipowazuru Alhamisi kuwajulia hali
Image: Ikulu Tanzania

Waliojeruhiwa wamekuwa wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa hali zao zinapokuwa zimeimarika na wengine wamekuwa wakipelekwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na kurejea nyumbani.

Maafa ya Hananga Manyara yalitokana na Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jumapili Novemba 3, na kusababisha sehemu ya mlima Hanang kumeguka hivyo kutokea maporomoko ya udongo uliozalisha tope liliharibu makazi ya watu na mali nyingine.