Jinsi watahiniwa wa KCPE 2023 wanaweza kujua shule ya upili ambayo watajiunga nayo

Wazazi sasa wanaweza kujua shule za upili ambapo watoto wao waliofanya mtihani wa KCPE 2023 wamechaguliwa kujiunga.

Muhtasari

•Machogu Jumatatu asubuhi alitoa matokeo ya upangaji wa shule katika Shule ya Lenana jijini Nairobi baada ya zoezi la upangaji wa nafasi wa wiki mbili kuendeshwa na wizara ya elimu.

•Mtu anaweza kupata kujua nafasi zao kupitia Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu nchini (KEMIS) kwa kutumia link http://kemis.education.go.ke/

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu
Image: EDU//MIN

Wazazi sasa wanaweza kujua shule za upili ambapo watoto wao waliofanya mtihani  wa Shule ya Msingi (KCPE 2023) wamechaguliwa kujiunga.

Watahiniwa wa KCPE 2023 wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mapema mwaka ujao.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu Jumatatu asubuhi alitoa matokeo ya upangaji wa shule katika Shule ya Lenana jijini Nairobi baada ya zoezi la upangaji wa nafasi wa wiki mbili kuendeshwa na wizara hiyo.

Wakati akiongoza upangaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2024. Machogu alisema wazazi wanapaswa kupakua barua za nafasi moja kwa moja kutoka kwa tovuti ya Wizara ya Elimu.

Alisema mara mtu anapoingia kwenye tovuti ya wizara, moja ni kutafuta Nafasi ya Kidato cha Kwanza ambapo watapata matokeo.

Zaidi ya hayo, mtu anaweza kupata kujua nafasi zao kupitia Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu nchini (KEMIS) kwa kutumia link http://kemis.education.go.ke/

"Ninawahakikishia Wakenya kwamba tovuti hii imejaribiwa na kuthibitishwa na ni sahihi kwa asilimia 100. Inaendelea kufanya kazi," alisema.

Machogu alisema uchaguzi wa shule waliochaguliwa ulitumika miongoni mwa vigezo vingine katika mchakato wa upangaji shule.

"Baadhi ya wanafunzi waliwekwa katika shule zenye hadhi sawa nje ya kaunti zao. Hii ni pamoja na wale kutoka kaunti zisizo na uwezo wa kutosha," CS alisema.

Kwa hivyo, mwanafunzi anaweza kuishia shule ya sekondari katika kaunti nyingine kwa sababu ya uhaba wa nafasi.

Zaidi ya hayo, Machogu aliwapa wazazi hakikisho kwamba hakutakuwa na nyongeza ya ada mwaka ujao watoto wao wanapojiunga na shule za upili.

"Serikali imejitolea kutoa elimu ya sekondari ya kutwa bila malipo ambayo inajumuisha mgao wa masomo na gharama za uendeshaji. Ada zinazotozwa katika shule za upili hazitabadilika mwaka wa 2024. Shule zitaendelea kupokea fedha kulingana na takwimu sahihi za uandikishaji,” alisema Machogu.