Waziri wa elimu Ezekiel Machogu atangaza tarehe ya kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2023

Muhtasari
  • KNEC ilifafanua kuwa kusahihishwa kwa mitihani ya KCSE bado kunaendelea, na kujitenga na ripoti za mtandaoni.
wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa KCPE 2023 katika jumba jipya la KNEC la Mitihani mnamo Novemba 23, 2023.
Waziri Ezekiel Machogu wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa KCPE 2023 katika jumba jipya la KNEC la Mitihani mnamo Novemba 23, 2023.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ametangaza tarehe ya kutolewa kwa matokeo ya Mtihani wa Sekondari ya Kenya (KCSE).

Kulingana na CS, matokeo yatatolewa katika wiki ya pili ya Januari 2024.

Machogu aliongeza kuwa ukusanyaji, uhakiki na uthibitishaji wa alama unaendelea kwa sasa.

Haya yanajiri baada ya Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC) mnamo Desemba 8,2023, kutoa taarifa ya kutupilia mbali ripoti zinazodai kuwa matokeo ya KCSE yatatolewa kabla ya Krismasi.

KNEC ilifafanua kuwa kusahihishwa kwa mitihani ya KCSE bado kunaendelea, na kujitenga na ripoti za mtandaoni.

"KNEC haijatoa kauli kama hiyo. Uwekaji alama wa KCSE unaendelea na matokeo yatatolewa yakiwa tayari," Baraza la Mitihani lilifafanua.

Wanafunzi wapatao 903,260 walifanya mitihani ya mwisho ya shule ya sekondari, iliyoanza Oktoba 23, 2023, na kukamilika Novemba 24, 2023.