Rita Waeni alinyongwa kabla ya kukatwa kichwa - Uchunguzi wa Maiti wabaini

"Pia tuliona baadhi ya mifupa imevunjika," alisema Oduor.

Muhtasari

•"Matokeo makuu yalikuwa kwamba kichwa kilikuwa kimekatwa kutoka shingo kwa kiwango cha C5 (vertebrae kwenye shingo)," Oduor alisema.

•Alisema kulikuwa na michubuko kichwani ambayo huenda ilitokana na kitu butu na baadhi ya mifupa kuvunjika shingoni.

Rita Waeni Muendo.
Rita Waeni Muendo.
Image: HISANI

Uchunguzi wa maiti ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT aliyeuawa Rita Waeni Muendo ulifichua kuwa alinyongwa na baadaye kukatwa kichwa.

Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor alisema hayo mnamo Alhamisi kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City, Nairobi.

Oduor pia alifichua kuwa kitu butu kilimkwaruza Waeni kichwani.

"Matokeo makuu yalikuwa kwamba kichwa kilikuwa kimekatwa kutoka shingo kwa kiwango cha C5 (vertebrae kwenye shingo)," Oduor alisema.

Kulikuwa na michubuko kichwani iliyosababishwa na kitu butu.

"Pia tuliona baadhi ya mifupa imevunjika," alisema Oduor alipokuwa akiwahutubia wanahabari.

"Ninaweza kuhitimisha kwa urahisi kwamba sababu ya kifo ilikuwa kunyongwa na kisha kukatwa kichwa na mwili wake kutupwa."

Alisema kulikuwa na michubuko kichwani ambayo huenda ilitokana na kitu butu na baadhi ya mifupa kuvunjika shingoni.

Kichwa kilikatwa shingoni, aliongeza.

Alhamisi, Familia ya Waeni aliyeuawa ilikuwa imetambua kichwa cha binadamu aliyepatikana kutoka kwa bwawa kuwa cha mwanamke huyo.

Hii ilifanywa kupitia paji la uso wake, nywele na malezi ya meno.

Hatua hiyo iliwapa wanapatholojia wakiongozwa na Chifu Oduor kibali cha kufanya uchunguzi wa kichwa  kama sehemu ya juhudi za kubaini jinsi alikufa mnamo Januari 13 katika ghorofa moja ya Roysambu, Nairobi.

Zoezi hilo lilifanywa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City kufuatia lile la awali lililokuwa limefanywa kwenye sehemu nyingine za mwili.

Familia hiyo ilikuwa imetambua blauzi ambayo ilikuwa imezungushiwa kichwani ilipogunduliwa katika bwawa la Kiambaa, Kaunti ya Kiambu.

Maafisa wa upelelezi wanashuku mauaji ya Waeni yalikuwa sehemu ya uchawi unaoendelea nchini.

Uchawi ni sehemu ya sababu kuu za mauaji nchini na timu ya uchunguzi ilisema ni sehemu ya nadharia wanazochunguza kama sababu ya mauaji ya kinyama.

"Inaonekana kama ibada ambayo nadhani ilichochewa na imani kama ya kidini," afisa mmoja anayefahamu suala hilo alisema.

Timu ya uchunguzi inataka kujua ikiwa kuna mauaji zaidi kama yale ya Waeni.