Seneta wa Busia Okiya Omutata ahusika katika ajali ya barabarani

Gari dogo la seneta huyo lililokuwa likielekea Busia liligongwa na lori lililokuwa likipanda mlima wa Ojola kuelekea Maseno.

Muhtasari

• Inaarifiwa kuwa lori hilo lilikuwa likipanda mlima lilipopata hitilafu ya breki na kuanza kurudi nyuma na kuligonga gari la Omtata upande wa kulia. 

Seneta wa Busia Okiya Omutata alihusika Katika Ajali ya BarabaraniAlhamisi jioni katika eneo la Ojolla kwenye barabara ya Kisumu - Busia. 

Gari dogo la seneta huyo lililokuwa likielekea Busia liligongwa na lori lililokuwa likipanda mlima wa Ojola kuelekea Maseno.

 Inaarifiwa kuwa lori hilo lilikuwa likipanda mlima lilipopata hitilafu ya breki na kuanza kurudi nyuma na kuligonga gari la Omtata upande wa kulia. 

Mkuu wa Trafiki Kanda ya Nyanza Allan Mwangi ambaye alithibitisha kisa hicho alisema kutokana na athari hiyo, gari la Seneta huyo liliharibika kidogo. 

Mwangi alisema Seneta huyo hakujeruhiwa wakati wa ajali hiyo na aliendelea na safari yake. 

Magari yote mawili yaliendeshwa hadi kituo cha polisi cha Maseno kwa uchunguzi zaidi.