Rais wa Kenya Ruto awaahidi pesa wanariadha

"Sasa tumerejesha hazina ya michezo ili kushughulikia masuala [ya] pekee ya michezo," amesema RaisWilliam Ruto.

Muhtasari

•Ruto alisema vifaa vyote vilivyoombwa wakati wa mazishi ya Ijumaa ya mshindi wa rekodi ya mbio za marathon Kelvin Kiptum vitatolewa.

Image: BBC

"Sasa tumerejesha hazina ya michezo ili kushughulikia masuala [ya] pekee ya michezo," amesema Rais wa Kenya William Ruto, akiongeza kuwa vifaa vyote vilivyoombwa wakati wa mazishi ya Ijumaa ya mshindi wa rekodi ya mbio za marathon Kelvin Kiptum vitatolewa.

"Tutarekebisha mfumo wetu wa zawadi - kwamba pia ziwe pesa kwa siku zijazo," pia ameahidi wakati wa hotuba yake kwa waombolezaji - akimaanisha maisha mafupi ya kikazi ya wanariadha wa juu ikilinganishwa na kazi zingine na matatizo ya kifedha wanayokabiliana nayo.

"Pesa zitawekwa katika mfumo wa pensheni kusaidia wanariadha baada ya kustaafu," rais aliongezea, akiitaka wizara ya michezo kutekeleza hili.

“Roho ya Kelvin ipumzike mahali pema peponi,” alimalizia.