Chagua bei yako na Tunukiwa: Chaguo zaidi na akiba kubwa

Piga *444# kwa urahisi, na utaletewa chaguzi za Ofa za Data au Ofa za Dakika.

Muhtasari
  • Ili kupata ofa hizi za kufana na kugundua hata zaidi, tembelea Programu ya MySafaricom au piga *444#.
  • Sasa unaweza kupata 1GB kwa shilingi 20 pekee, zenye uhalali wa kutumika kwa saa 1, kuhakikisha kuwa unaweza kujivinjari kwa maudhui yako ya moyoni.

Wakenya ndio watafutaji wakubwa wa ofa. Iwe kwa mama mboga kununua mboga au kujadiliana nauli ya basi na makanga, nia yao mara nyingi huwa pale kwenye bei nzuri, au bei rahisi Zaidi kwa kila kitu.

 Safaricom inaelewa kuwa Wakenya wanashughulikia majukumu mengi ya kifedha na mapato finyu na wanatoa data na chaguo za kupiga simu zinazoruhusu Wakenya kufanya mengi kwa bei nafuu na zinapatikana kwa urahisi.

Ofa za Tunukiwa kutoka zimesawazishwa hata zaidi, na zinatoa thamani na chaguo zaidi kuliko hapo awali. Iwe unatafuta kuungana na wapendwa wako kupitia kupiga simu au kusalia mtandaoni, ofa hizi zipo kwa ajili yako. Hivi ndivyo utakavyoweza kuzifikia;

Piga *444# kwa urahisi, na utaletewa chaguzi za Ofa za Data au Ofa za Dakika. Kutoka hapo, chagua ofa inayokidhi mahitaji yako na ulipe kwa kutumia Airtime, M-PESA, au Bonga Points.

 Vinginevyo, ikiwa unayo programu ya mySafaricom, unaweza kuchagua chaguo la Tunukiwa na uchague kati ya vifurushi vya mtandao, vifurushi vya dakika, au mchanganyiko, kuhakikisha unapata kile unachohitaji.

Kwa nyakati zile unapotaka kuwasiliana na mpendwa au kuungana tena na rafiki uliyepoteleana naye kwa muda mrefu, kuna ofa nyingi zinazokungoja. Kwa mfano, usikose nafasi ya kupata dakika 30 za muda wa kupiga simu kwa shilingi 20 tu, zitakazohitajika kutumika ndani ya saa tatu.

Na linapokuja suala la data, kila bundle huleta tofauti, inakuruhusu kuokoa kwa kiasi kikubwa kupitia ofa za Tunukiwa kutoka Safaricom.

Sasa unaweza kupata 1GB kwa shilingi 20 pekee, zenye uhalali wa kutumika kwa saa 1, kuhakikisha kuwa unaweza kujivinjari kwa maudhui yako ya moyoni.

Iwe uko kwenye TikTok, Instagram au LinkedIn, ofa hizi zinakuruhusu kupitia katika majukwaa mbalimbali unayoyapenda bila wasiwasi.

Ili kupata ofa hizi za kufana na kugundua hata zaidi, tembelea Programu ya MySafaricom au piga *444#.

Chagua Bei Yako na Tunukiwa – na unufaike zaidi kutokana na matumizi yako ya Safaricom.