Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi aaga dunia

Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serekali ya Awamu ya Pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985. Alizaliwa tarehe 5 mei, 1925.

Muhtasari

• Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa rais huyo wa awamu ya pili, amefariki katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam siku ya leo.

• Rais huyo wa zamani anatarajiwa kuzikwa siku ya tarehe 2 machi huko visiwani Zanzibar.

• Aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar mwaka 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970.

Marehemu Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.
Image: BBC

Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ameaga dunia.

Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serekali ya Awamu ya Pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985. Alizaliwa tarehe 5 mei, 1925.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa rais huyo wa awamu ya pili, amefariki katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam siku ya leo.

Alikua akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya Mapafu.

‘’Hayati mzee Ali Hassan Mwinyi, amekua akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana nchini Uingereza, na baadaYe kurejea nchini alipokua akiendelea na matibabu katika hospitali ya Mzena, hadi umauti ulipomfika’’

Aidha rais Samia ameongeza kuwa Tanzania itaombeleza kwa siku saba.

Rais huyo wa zamani anatarajiwa kuzikwa siku ya tarehe 2 machi huko visiwani Zanzibar.

Katika safari yake ya kisiasa, Ali Hassan Mwinyi alijiunga na chama cha Afro Shiraz(ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbali mbali za serekali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar mwaka 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya.

Alikuwa Waziri Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri.

Mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.