5 wafariki, wengine 18 wajeruhiwa katika ajali ya barabarani Bomet

Watu 18 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Tenwek.

Muhtasari

•Watano walifariki  Jumatatu katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Olonguruone-Silibwet, katika kaunti ya Bomet.

•Gari hilo na trekta zilipelekwa hadi kituo cha polisi cha Bomet kwa hatua zaidi za polisi.

eneo la tukio la ajali
Image: HISANI

Watu wapatao watano walifariki  Jumatatu katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Olonguruone-Silibwet, katika kaunti ya Bomet.

Ajali hiyo iliyohusisha matatu na trekta iliwaacha 18 wakiwa wamejeruhiwa.

"Ilitokea kwamba dereva alikuwa akiendesha gari lake kutoka Olenguruone likielekea Bomet General na kufika eneo la ajali, dereva wa matatu alishindwa kukaa kwenye njia yake na kugonga trekta," ripoti ya polisi ilifikia Radio Jambo ilisomeka.

Watu 18 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Tenwek.

Gari hilo na trekta zilipelekwa hadi kituo cha polisi cha Bomet kwa hatua zaidi za polisi.

Tangu Januari hadi Februari 2024, ajali za barabarani kote nchini zimegharimu maisha ya watu 649, Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama ilisema.

Takwimu ni ongezeko ikilinganishwa na 623 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa 2023.

Watembea kwa miguu wanaongoza kwa vifo kwa 252, ikilinganishwa na 190 iliyorekodiwa mwaka jana.

Waendesha pikipiki walirekodi vifo 152 na kuashiria kupungua kidogo ikilinganishwa na 177 mnamo 2023.

Mnamo 2024, angalau abiria 125 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani ikilinganishwa na 114 mnamo 2023.

Madereva 43 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani. Huu ni upungufu ikilinganishwa na 59 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Abiria wa nyuma walirekodi vifo 61 ikilinganishwa na 71 vilivyoshuhudiwa mwaka jana.