Serikali yatangaza Jumatano, Aprili 10 kuwa Sikukuu ya Umma

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali, likizo hiyo itatumika kuadhimisha Eid-ul-Fitr.

Muhtasari

•Waziri wa Masuala ya Ndani Kithure Kindiki ametangaza siku ya Jumatano, Aprili 10, 2024 kuwa sikukuu ya umma.

Waziri wa usalama na maswala ya ndani Kithure Kindiki
Waziri wa usalama na maswala ya ndani Kithure Kindiki
Image: HISANI

Waziri wa Masuala ya Ndani Kithure Kindiki ametangaza siku ya Jumatano, Aprili 10, 2024 kuwa sikukuu ya umma.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali, likizo hiyo itatumika kuadhimisha Eid-ul-Fitr.

"Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, natangaza Jumatano, Aprili 10 2024, itakuwa sikukuu ya kuadhimisha Idd-ul-Fitr," Kindiki alisema.

Eid-ul-Fitr ni sikukuu kuu ya kidini kwa Waislamu inayoashiria mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan ambao ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

Sherehe hiyo huanza kwa sala maalum, inayojulikana kwa jina la Eid, inayoswaliwa mapema asubuhi baada ya kuonekana kwa mwezi mpevu.