Ruto atuma risala za rambi rambi kwa familia ya Tom Ojeinda kufuatia kifo cha mama yake

"Alikuwa mpenda elimu na mwanamke aliyejitolea ambaye ushauri wake umebadilisha maisha ya watu wengi," Rais alisema.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake  kwenye ukurasa wake rasmi wa X, Ruto alisema Mama Agnetta alikuwa mwalimu mashuhuri.
RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto ametuma risala zake za rambirambi kwa Prof Tom Ojienda kufuatia kifo cha mamake Agnetta Okello.

Katika taarifa yake  kwenye ukurasa wake rasmi wa X, Ruto alisema Mama Agnetta alikuwa mwalimu mashuhuri.

"Alikuwa mpenda elimu na mwanamke aliyejitolea ambaye ushauri wake umebadilisha maisha ya watu wengi," Rais alisema.

"Mawazo na sala zetu ziko kwa familia na marafiki katika wakati huu mgumu. Pumzika kwa Amani, Mama Agnetta."

Ojienda alimshukuru Rais kwa ujumbe wake wa rambirambi.

"Kwa niaba ya familia yangu na mimi mwenyewe, tunakushukuru Mheshimiwa Rais kwa ujumbe wako wa rambirambi," alisema X.

"Pia tunashukuru kwa msaada wako na maneno ya kutia moyo katika wakati huu mgumu."