Mwanamke aanguka na kufariki bafuni Pangani

Kulingana na polisi, Sophia Wangari alikuwa akioga bafuni yake mnamo Juni 4 alipoanguka.

Muhtasari

•Mtu wa familia aliyekuwa ndani ya nyumba alisikia anguko hilo na kukimbia pale.

•Alikimbizwa katika Hospitali ya Gurunanak ambako alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Rip
Rip
Image: HISANI

Maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 47 alifariki baada ya kuanguka katika bafu la nyumba yake iliyo eneo la Pangani, Nairobi.

Kulingana na polisi, Sophia Wangari alikuwa akioga bafuni yake mnamo Juni 4 alipoanguka.

Mtu wa familia aliyekuwa ndani ya nyumba alisikia anguko hilo na kukimbia pale.

Alimkuta akijaribu kusimama na akamjulisha kuwa anajisikia vibaya.

Mwanafamilia huyo aliambia polisi kwamba Wangari alianguka tena na kupoteza fahamu.

Alikimbia kumsaidia bila mafanikio.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Gurunanak ambako alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Polisi waliouona mwili huo walisema alikuwa na jeraha kwenye paji la uso ambalo huenda lilisababishwa na kuanguka.

Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti na uchunguzi mwingine.