Mashambulizi dhidi ya maafisa wamahakama hayakubaliki- Ruto asema huku akimuomboleza Kivuti

Hakimu aliaga dunia baada ya polisi kufyatua risasi katika mahakama ya Makadara wiki jana na kuwajeruhi maafisa wengine watatu.

Muhtasari
  • Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi katika Kaunti ya Kisumu aliuawa kwa kupigwa risasi papo hapo na maafisa wenzake.
Monica Kivuti
Image: Facebook

Rais William Ruto amewataka polisi kuwalinda maafisa wa mahakama akisema yaliyompata Hakimu Mkuu wa Makadara Monicah Kivuti 'hayafai kutokea tena'.

Hakimu aliaga dunia baada ya polisi kufyatua risasi katika mahakama ya Makadara wiki jana na kuwajeruhi maafisa wengine watatu.

Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi katika Kaunti ya Kisumu aliuawa kwa kupigwa risasi papo hapo na maafisa wenzake.

Rais aliwaonya maafisa wa polisi dhidi ya kuwatumia bunduki watu wanaofaa kuwalinda akisisitiza kuwa vitisho kwa maafisa wa mahakama havikubaliki.

"Ninaungana na familia, marafiki na idara ya mahakama kuomboleza kifo  cha Mheshimiwa Monica Kivuti ambaye alikuwa akihudumu kama Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Makadara,'' Rais Ruto alichapisha kwenye akaunti yake ya X .

"Makabiliano, vitisho au mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya maafisa wa mahakama hayakubaliki, ni jinai na ni dharau kwa utawala wa sheria."

Rais alisema kuwa polisi wapo ili kuwahakikishia Wakenya usalama wa kutegemewa.

"Kwa hali yoyote wasiache jukumu hili muhimu au kugeuka kutoka kwa jukumu lao la ulinzi na kuwa tishio kwa usalama na usalama wa watu," alisema.

Alisema kilichotokea Kivuti hakikubaliki na hakipaswi kutokea tena.

"Ninaomba polisi wahakikishe usalama wa maafisa wetu wa mahakama kila wakati wanapotekeleza majukumu yao. Tumempoteza mtaalam wa mahakama ambaye alitumikia Wakenya kwa kujitolea. Bado alikuwa na mengi ya kutoa kwa nchi yetu," Rais alisema.

"Nakuombea Mwenyezi Mungu akupe nguvu za kustahimili msiba huu, na kukufariji kwa faraja ya Mwenyezi Mungu," alisema.