'Amekuwa mama yetu,' DP Gachagua amuomboleza dada yake mkubwa

Naibu Rais alitangaza kifo cha dada yake kupitia kwenye ukurasa wake rasmi ya X

Muhtasari
  • “Pole zangu nyingi kwa mume wake, watoto wake na wajukuu. Wiki hii ni ngumu sana kwangu kama kiongozi wa kitaifa na mwanafamilia. Bwana apone taifa letu na familia,” aliongeza.
LEAH WANGUI
Image: RIGATHI GACHAGUA/ X

Naibu Rais Rigathi Gachagua amempoteza dadake mkubwa Leah Wangari Muriuki.

Naibu Rais alitangaza kifo cha dada yake kupitia kwenye ukurasa wake rasmi ya X

“Leah amekuwa mama yetu wa familia ; ameitunza vyema familia kubwa ya Gachagua baada ya kifo cha baba yetu na mama zetu wawili,” alisema huku akitangaza kifo chake.

DP alisema wamesikitishwa sana na kifo cha mkuu wa familia.

Aliongeza;

“Pole zangu nyingi kwa mume wake, watoto wake na wajukuu. Wiki hii ni ngumu sana kwangu kama kiongozi wa kitaifa na mwanafamilia. Bwana apone taifa letu na familia,” aliongeza.