Polisi wakiri kumkamata kimakosa mwanahabari Macharia Gaitho, wafichua waliyekuwa wakitafuta

Idara ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisisitiza kuwa hawalengi wanahabari

Muhtasari

•NPS imekiri kukamatwa kwa mwanahabari mkongwe Macharia Gaitho mnamo  kulikuwa na kisa cha utambulisho wa kimakosa.

•Kulingana na polisi, mshawishi huyo maarufu wa mitandao ya kijamii yuko chini ya uchunguzi unaoendelea.

alikamatwa Jumatano asubuhi
Mwanahabari mkongwa Macharia Gaitho alikamatwa Jumatano asubuhi
Image: HISANI

Idara ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imekiri kwamba kukamatwa kwa mwanahabari mkongwe Macharia Gaitho mnamo Jumatano asubuhi kulikuwa na kisa cha utambulisho wa kimakosa.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, NPS ilifafanua kwamba hawakumaanisha kumkamata mwanahabari huyo mkongwe, bali walikuwa wakimlenga mwanablogu maarufu wa kisiasa, Francis Gaitho.

Kulingana na polisi, mshawishi huyo maarufu wa mitandao ya kijamii yuko chini ya uchunguzi unaoendelea.

"Huduma ya Kitaifa ya Polisi ingependa kufafanua kwa umma kwamba asubuhi ya leo, tulimkamata mwanahabari Macharia Gaitho katika kesi ya utambulisho kimakosa, iliyokusudiwa kumkamata Francis Gaitho ambaye ni mchunguzi wetu," NPS ilisema katika taarifa.

Idara ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisisitiza kuwa hawalengi wanahabari, kama ilivyodaiwa baada ya kisa hicho cha kushtua Jumatano asubuhi.

 "Tunasisitiza kwamba kama Huduma, hatulengi waandishi wa habari kwa njia yoyote, na tukio la leo ni la kusikitisha sana. Huduma ya Polisi ya Kitaifa inasalia kujitolea kufanya kazi na vyombo vya habari huku tukitekeleza jukumu letu la kukuza uwajibikaji na uwazi,’ walisema.