Rais Ruto atia sahihi Sheria ya Marekebisho ya Bajeti ya Kifedha

Licha ya vikwazo vya kifedha, sheria hii mpya inahakikisha fedha kwa maeneo na sekta kadhaa muhimu.

Muhtasari

•Sheria hii inatenga takriban shilingi bilioni 20 kusaidia wakulima na kuboresha uzalishaji na ufanisi wa kilimo.

•Sheria hii mpya inapendekeza kupunguzwa kwa matumizi ya mara kwa mara na ya maendeleo kwa matawi matatu ya serikali, tume za katiba na ofisi huru

Rais William Ruto
Image: MAKTABA

Rais William Ruto mnamo Jumatatu alitia sahihi  Sheria ya Marekebisho ya Bajeti ya Kifedha baada ya kupitishwa na Bunge la Kitaifa mnamo Julai 31, 2024.

Licha ya vikwazo vya kifedha, sheria hii mpya inahakikisha fedha kwa maeneo na sekta kadhaa muhimu.

Sheria hii inatenga takriban shilingi bilioni 20 kusaidia wakulima na kuboresha uzalishaji na ufanisi wa kilimo.

Kwa ajili ya marekebisho ya elimu, sheria hii inatoa shilingi bilioni 120.7, ikiwa ni pamoja na fedha za kuthibitisha walimu wote wa Shule za Sekondari za Kati na shiling milini bilioni 31.3 kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Zaidi ya hayo, Sheria hii inatoa shilingi bilioni 16.2 kwa marekebisho ya sekta ya afya na kuendeleza Upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wote.

Sheria hii pia inashughulikia ongezeko la mishahara kwa maafisa wa usalama, ikitenga shilingi bilioni 3.5 kuboresha malipo ya maafisa wa mashirika mbalimbali, kulingana na mapendekezo ya Kamati ya Kitaifa ya Marekebisho ya Polisi.

Aidha, Sheria hii mpya inapendekeza kupunguzwa kwa matumizi ya mara kwa mara na ya maendeleo kwa matawi matatu ya serikali, tume za katiba na ofisi huru.

Kwa ujumla, bajeti ya Serikali ya Kitaifa imepunguzwa kwa shilingi bilioni 145.7 ikiwa ni pamoja na shilingi bilioni 40 kwa matumizi ya mara kwa mara na shilingi bilioni 105 kwa matumizi ya maendeleo.

Katika kupunguziliwa mbali, bajeti ya Utawala imepunguziliwa kwa shilingi bilioni 139.81  huku bajeti ya Bunge ikipunguzwa kwa shilingi bilioni 3.7 na ile ya Mahakama kwa shilingi bilioni 2.1.

Bajeti ya Ikulu na Ofisi ya Naibu Rais imepunguziliwa kila mmoja kwa shilingi bilioni 6, wakati bajeti ya Hazina ya Taifa imepunguziliwa kwa shilingi bilioni 7.

Bajeti ya Wizara ya Afya imepunguziliwa kwa shilingi bilioni 6.9, na bajeti ya Barabara na Usafiri imepunguziliwa kwa shilingi bilioni 17.3.