Mmoja afariki na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya lori la gesi

Lori hilo lililokuwa lilikuwa lisafirisha gesi liligonga magari kadhaa ikiwa ni pamoja na matatu ya kubeba watu 14 ambayo ilibingiria bondeni.

Muhtasari

•  Kulingana na polisi, lori hilo lililokuwa lilikuwa lisafirisha gesi liligonga magari kadhaa ikiwa ni pamoja na matatu ya kubeba watu 14 ambayo ilibingiria bondeni. 

Lori la gesi ya LPG lililohusika katika ajali eneo la Mai Mahiu mnamo Septemba 11, 2024 Picha: HISANI.
Lori la gesi ya LPG lililohusika katika ajali eneo la Mai Mahiu mnamo Septemba 11, 2024 Picha: HISANI.

Mtu mmoja amethibitishwa kufariki na wengine 12 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa likisafirisha gesi aina ya LPG kupoteza udhibiti katika eneo la Mai Mahiu. 

Kulingana na polisi, lori hilo lililokuwa lilikuwa lisafirisha gesi liligonga magari kadhaa ikiwa ni pamoja na matatu ya kubeba watu 14 ambayo ilibingiria bondeni. 

Matatu hiyo ilikuwa ikielekea Rongo kwa mazishi wakati kisa hicho kilipotokea.

Tutakuletea habari zaidi...