Tume ya maadili na kupambana na ufisadi yavamia makaazi ya wakuu wa KeRRA

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi yavamia makaazio ya viongozi wawili wakuu wa KeRRA kwa tuhuma za ufisadi

Muhtasari

•Tume ya maadili na kupambana na ufisadi ilivamia maakazi ya maafisa wawili wa KeRRA kwa tuhuma za ulaghai wa tenda na ufajaji wa fedha.

•Mutambu Kilonzi na Eng. Joseph Murage Kimata wanatuniwa na kupeana tenda za mamilioni kwa kampuni zinazomilikiwa na familia na mfanya kazi mwenza wa zamani,mfululizo.

Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
EACC Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
Image: MAKTABA

Maafisa wa tume ya maadaili ankupambana na ufisadi (EACC) wamevamia makaazi ya mameneja wakuu wawili wa shirika la ujenzi wa barabara KeRRA,kwa tuhuma za ufisadi wa mamilioni ya pesa na utwaaji wa mali ya mamilioni  kwa njia isiyo sahihi.

Mhasibu wa Tume hiyo  mkoa wa kaunti ya Lamu Mutambu Kilonzi pamoja na mratibu wa kaunti ya klirinyaga Eng. Joseph Murage Kimata walituhumiwa kwa matumizi mabaya ya pesa za kiwango cha Milioni 500 kwa njia ya ulaghai wa ununuzi wa tenda za urekebishaji wa barabara na utengezaji.

Maafisa wa tume hiyo wallivamia nyumbani kwake  Kilonzi shughli ambayo iliendeshwa sawia nyumbani kwake Kimata maeneo ya Kirinyaga.Maafisa haop walifanikiwa kupata ushahidi tosha kutokana na tuhuma hizo.Aidha tume hiyo sasa imewataka wawilihao kuregesha mali hiyo kwa serikali na kufunguliwa mashtaka.

Kilonzi alituhumiwa kwa kutumia njia zisizofaa na kufanya malipo ya shilingi milioni 216 kwa kampuni ambazo zinamilkiwa na bibi yake na jamaa zake.

Kwa upande wake Kimata,alituhumiwa kwa kutoa tenda ya zaidi ya milioni 311 kwa klampuni nne ambazo zinamilkiwa na mfanya kazi mwenza wa zamani.

Kimata,amabye aliwahi kufanya kazi na KeRRA kama mratibu wa Kaunti ya Kiambu,kabla ya kupelekwa katika kaunti ya Kirinyaga,aliripotiwa kwamba alifanya malipo ya shilingi 311,125,109.90 kwa Fidelis Mumbi.

Ms. Mumbi ambaye ni mratibu wa kampuni nne na hapo awali alifanya kazi na kimata katika ofisi za KeRRA ,Kiambu.

Wawili hao sasa wamnatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ulaghai na ufujaji wa pesa.