Shule ya St. Monica Kitale yafungwa ghafla

Hii ni kutokana na wanafunzi kuandamana Jumapili asubuhi wakilalama kutokula chajio kwa siku tatu

Muhtasari

• Wanafunzi wanataka kuondolewa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo bi. Grace Anyango kwa madai ya usimamizi mbaya wa shule hiyo.

• Wazaziwanatakiwa kuwachukua wanao kutoka shule; taarifa kamili kutoka usimamizi wa shule hiyo unasubiriwa.

Image: hisani

Shule ya upili ya wasichana ya St. Monica Kitale katika kaunti ya Trans Nzoia imefungwa ghafla baada ya wanafunzi kuandamana wakimtaka mwalimu mkuu wa shule hiyo kuhamishwa.

Maandamano hayo ya wanafunzi ya Jumapili asubuhi yawefanywa wanafunzi wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule kutoka kwa mwalimu mkuu Bi. Grace Anyango.

Inaripotiwa kuwa baadhi ya wanafunzi wamelalamikia maswali mengi wanayokumbana nayo shuleni humo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zingali kudhibitishwa na kutuo hiki, inadaiwa kuwa wanafunzi wanalalamikia kutokula chajio kwa siku tatu kati ya maswala mengine ikiwemo mazingira mabaya ya kusoma na utumizi mbaya wa hela.

Kinachotarajiwa sasa ni taarifa kutoka kwa bodi ya usimamizi wa shule hiyo kuelezea hatua itakayochukuliwa.

Katika video inayosambaa mtandaoni, wanafunzi wa shule hiyo wanaoenekana wakiwa wamebeba mifuko yao wakitoka nje ya lango kuu ya shukle hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wamechukuliwa na wazazi wao huku wazazi ambao hawajawachukua wanao wakitakiwa kufika shuleni humo kuwachukua wanao.

Shule yaupili ya wasichana ya St. Monica inakuwa shuke ya pili chini ya wiki kufungwa kwa muda usiojulikana baada ya shule ya upili ya Dagoretti kufungwa kufuatia utovu wa utulivu wakati wa mchuano wa mpira wa vikapu baina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha nne.