logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nitashauriana kwa upana na kutangaza mwelekeo - Raila Odinga

iongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akizungumza leo amesema kwamba siku chache zijazo atapeana mwelekeo kwa wafwasi wake.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri24 February 2025 - 16:02

Muhtasari


  • Odinga ambaye alikuwa miongoni mwa wawaniaji watatu wa kiti hicho huku akiwakilisha kenya alipoteza kwa mwenzake wa Djibout Mahmoud Ali Youssouf baada kumaliza wa pili.
  • Mwanasiasa huyo pia ameondoa dukuduku kutokana na madai kwamba serikali ilitumia bilioni 13 kufadhili kampeni zake.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akizungumza leo Februari 24, amesema kwamba siku chache zijazo atapeana mwelekeo kwa wafwasi wake.

Odinga amesema kwamba mwanzo atafanya utafiti na kushaurina na wengine ili kufanya maamuzi  kwa siku za hivi karibuni.

Mwanasiasa huyo maarufu ambaye amekuwa kwenye ulingo wa siasa kwa zaidi miongo mitatu sasa amezungumza  kwa mara ya kwanza kabisa tangu kukamilika kwa uchaguzi wa kuwania kuwa mwenyekiti wa umoja wa Africa 'AU' 

Odinga ambaye alikuwa miongoni mwa wawaniaji watatu wa kiti hicho huku akiakilisha kenya alipoteza kwa mwenzake wa Djibout Mahmoud Ali Youssouf baada kumaliza wa pili.

Waziri mkuu huyo wa zamani ambaye ana wafwasi zaidi ya milioni sita kulingana na uchaguzi uliopita amewataka wafwasi wake kutokuwa na wasiwasi akiahidi kuwa atapeana mwelekeo siku za hivi karibuni.

"Nimerudi nyumbani, nitaenda kukutana na marafiki zangu, wafwasi wangu,  nitafanya mashauriano mbalimbali kuhusu kinachoendelea mbele, na kwa muda usiokuwa mrefu nitatangaza mwelekeo," odinga amesema.

Wakati huo huo pia amempongeza rais William Ruto kwa kusimama na yeye wakati wa kampeni za umoja wa Afrika na pia akawapongeza wapinzani wake ambao alikuwa akibishana nao hasa aliyetwaa ushindi Mahmoud Youssouf pamoja na wakenya ambao walimuunga mkono.

"Pia nataka kushukuru viongozi wengine kutoka Africa nzima ambao walitupigia kura, kuna wale walisimama na sisi mpaka wakati wa mwisho. na kama tungetaka tungesimamisha uchaguzi, maana ilihitajia thuluthi mbili ili kuchaguliwa, hatungepata kiongozi kama ningeendelea. Nashukuru wale ambao pia hawakupiga kura kwetu maana ni haki yao kidemokrasia. niliwashukuru wapinzani wangu kutoka Madagascar na Djibouti, Nashukuru pia rais na timu yake kwa kunishika mkono," aliongeza kiongozi huyo wa Azimio.

Odinga pia ameeleza kwamba maamuzi ya kwenda kuwania nafasi ya kuwa mwenyekiti wa AU, yalikuwa maamuzi yake na raisi Williamu ruto alikuja tu kumusaidi wakati akiwa tayari amefanya maamuzi. Na kwa vile alikuwa anakwenda huko kuwakilisha Kenya serikali ilisitahili kufanya hivyo.

Namshukuru rais William Ruto kwa kusimama upande wangu. Hakuniuliza niende kupigania nafasi hiyo. nilitangaza mwenyewe kwamba nitakwenda kupigania nafasi hiyo. Ruto alikuja kunisaidia tu baada ya mimi kutangaza kuwania nafasi hiyo naye akaja kunisaidia.

Mwanasiasa huyo pia ameondoa dukuduku kutokana na madai kwamba serikali ilitumia bilioni 13 kufadhili kampeni zake.

"Mtu mahali anaongelea bilioni 13 zilitumika kufanya kampeni ya Raila, sijui anaishi dunia gani hajui biliioni ni nini, bilioni yote ya kufanyia nini. Pesa ambazo zilitumika ni kidogo tu za kusafiri, tulikula kile tulipewa mahali tulienda. Nchi nyingi za Afrika zilikuwa na upendo walitupa mahali pa kulala," Odinga alisema.

 

 

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved