Ndege mbili zagongana Nairobi, watu wawili wafariki huku 44 wakinusurika kifo (+picha)

Wengine takriban 44 walinusurika bila majeraha katika kisa hicho cha Jumanne asubuhi.

Muhtasari

•Tukio hilo lilihusisha ndege aina ya Dash 8  iliyokuwa ikielekea Diani ikiwa na abiria 44 na wafanyikazi na ndege aina ya Cessna.

•Ndege hiyo aina ya Cessna ilianguka katika bustani hiyo huku Dash 8 ikifanikiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Wilson.

ya ndege katika Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi mnamo Machi 5, 2023
Mabaki ya ndege katika Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi mnamo Machi 5, 2023
Image: HISANI

Takriban watu wawili walifariki wakati ndege mbili ziligongana katika Hifadhi ya Kitaifa ya Nairobi.

Wengine takriban 44 walinusurika bila majeraha katika kisa hicho cha Jumanne asubuhi.

Tukio hilo lilihusisha ndege aina ya Dash 8 yenye nambari ya usajili 5YSLK, mali ya Safari Link iliyokuwa ikielekea Diani ikiwa na abiria 44 na wafanyikazi na ndege aina ya Cessna.

Ndege ya Cessna nambari  5YNNJ ilikuwa na watu wawili na ilikuwa kwenye kikao cha mafunzo wakati tukio hilo lilipotokea, polisi walisema.

Ndege hiyo aina ya Cessna ilianguka katika bustani hiyo huku Dash 8 ikifanikiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Wilson.

Ndege zote mbili zilitoka katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, maafisa walisema. Afisa mmoja alisema kulikuwa na watu wawili walioaga katika ajali hiyo.

"Safarilink Aviation inapenda kutoa taarifa kwamba asubuhi ya leo saa nne kasorobo kwa Saa za Ndani, ndege yetu nambari 053 ikiwa na abiria 39 na wafanyakazi 5 waliokuwa wakielekea Diani ilipata kishindo kikubwa mara baada ya kupaa."

“Wahudumu waliamua kurejea mara moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Nairobi-Wilson kwa ukaguzi na tathmini zaidi na walitua salama. Hakukuwa na majeruhi walioripotiwa,” opereta alisema.

Taarifa yao iliongeza vyombo husika vimearifiwa na pamoja na Safarilink Aviation wanachunguza tukio hilo.

Hili ni tukio la hivi punde zaidi kuhusisha ndege zinazotoka katika uwanja huo. Uwanja wa ndege hushughulikia zaidi wale walio chini ya mafunzo.