(Picha) Kutana na familia ya gavana wa Nairobi Johnson Sakaja

Johnson Sakaja ameapishwa kama gavana wa nne wa Nairobi.

Muhtasari

•Sakaja aliapishwa kama gavana wa nne wa Nairobi mwendo wa saa tano asubuhi ya Alhamisi katika ukumbi wa KICC. 

•Aliwasili katika ukumbi huo mwendo wa saa nne unusu asubuhi akiwa ameandamana na familia yake. 

akiwasili katika ukumbi wa KICC kwa hafla ya kuapishwa mnamo Alhamisi Agosti 25, 2022.
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja akiwasili katika ukumbi wa KICC kwa hafla ya kuapishwa mnamo Alhamisi Agosti 25, 2022.
Image: EZEKIEL AMINGA

Aliyekuwa seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ameapishwa kama gavana wa nne wa kaunti hiyo.

Sakaja aliapishwa mwendo wa saa tano asubuhi ya Alhamisi katika ukumbi wa KICC. 

Hakimu Roselyn Aburili ndiye aliyesimamia hafla hiyo.

Mamia ya wageni waalikwa wakiwemo wanasiasa mashuhuri walishuhudia kuapishwa kwa Sakaja moja kwa moja.  Rais mteule William Ruto ni miongoni mwa wageni waliokuwa wamehudhuria.

Sakaja aliwasili katika ukumbi huo mwendo wa saa nne unusu asubuhi akiwa ameandamana na familia yake. Alikuwa amevalia suti ya bluu bahari na tai nyekundu huku wanawe wakiwa na suti ya kijivu na tai nyeusi.

Mke wake Beatrice Sakaja, wanawe wawili waliongozana naye kwenye hafla hiyo. Binti aliyekuwa pamoja nao sio wake.

awasili katika ukumbi wa KICC akiwa ameandamana na watoto wake.
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja awasili katika ukumbi wa KICC akiwa ameandamana na watoto wake.
Image: EZEKIEL AMINGA
Wanawe gavana Johnson Sakaja
Image: EZEKIEL AMINGA
Wanawe Sakaja katika ukumbi wa KICC mnamo Agosti 25, 2022
Image: EZEKIEL AMINGA
katika hafla ya uapisho mnamo Agosti 25, 2022.
Gavana Johnson Sakaja , Naibu wake James Muchiri, hakimi Caroline Kabucho, Bi Beatrice Sakaja (nguo ya manjano) katika hafla ya uapisho mnamo Agosti 25, 2022.
Image: EZEKIEL AMINGA