Waziri Machogu kutangaza matokeo ya KCPE leo adhuhuri

Watahiniwa 1,244, 188 wa KCPE 2022 wanatarajiwa kujua matokeo yao leo.

Muhtasari

•Machogu atatangaza jinsi watahiniwa wa KCPE 2022 walivyofanya baada ya kuwasilisha matokeo yao kwa rais William Ruto.

•Mtihani wa KCPE ulifanywa kati ya Novemba 28 na Novemba 30 ambapo watahiniwa 1,244, 188 walijaribiwa.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu.
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu.
Image: Facebook

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCPE 2022 leo Jumatano.

Machogu atatangaza jinsi watahiniwa wa KCPE 2022 walivyofanya katika Mtihani House, jijini Nairobi baada ya kuwasilisha matokeo yao kwa rais William Ruto. Ataandamana na bodi ya kusimamia mitihani ya KNEC.

Kulingana na KNEC, matokeo hayo yatatangazwa mwendo wa adhuhuri.

Mtihani wa KCPE 2022 ulifanywa kati ya Novemba 28 na Novemba 30 ambapo watahiniwa 1,244, 188 walijaribiwa.

Takriban wanafunzi 1, 287,597 wa daraja ya sita pia walifanya mitihani yao ya KPSEA katika kipindi hicho. Waziri Machogu anatarajiwa kuwapa mwelekeo baada ya kutangaza matokeo ya KCPE 2022.