Brazil kukabana koo na Argentina kwenye nusu fainali

Dimba la copa America limefikia kwenye awamu ya nusu fainali. Raudi hii, Brazil anamkaribisha Argentina kwenye nusu fainali ya kwanza huku Chile ikakabana koo na Peru. Selecao ilibandua paraguay kupitia kwenye matuta ya penalti huku Argentina ikiadhibu venezuela 2-0.

Brazil haijawahi poteza mechi yoyote dhidi ya Argentina ikiwa nyumbani kwao. Pamoja na hayo, Brazil imelitwaa taji la copa ametrica mara zote ilipokuwa mwenyeji wa shindano hilo.

Kwenye uwanja huo huo ndipo ambapo Brazil ilipopteza mechi yake dhidi ya Ujerumani 7-1 kwenye nusu fainali ya kombe la dunia. Mechi yao ya mwisho kwenye uwanja huo ilikuja dhidi ya Argentina ambapo Brazil walipata ushindi rahisi wa magoli matatu bila jibu.

Ikiongozwa naye Lionel Messi, Argentina itakuwa mawindoni kutafta taji lao la kwanza kwa miaka 26 iliopita. Argentina imepoteza fainali mbili ilizoshiriki mikononi mwa Chile kupitia njia ya penalti.

Ikiongozwa naye winga wa Manchester United, Alexis Sanchez, Chile watakuwa wenyeji wa peru kwenye nusu fainali ya pili. Chile ilipata ushindi kupitia njia ya penalti dhidi ya Colombia. Chile ndio mabingwa watetezi wa taji hili huku wakiwa wamelitwaa taji hili mara mbili mfululizo.

Kwa upande mwingine, Peru ilibandua Uruguay yake Luis Suarez kupitia njia ya penalti baada ya sare tasa. Uruguay walilazimishwa kwenda  mapenalti ambapo mshambulizi wa klabu ya Barcelona Luis Suarez alipoteza mkwaju wake hivo kuipa Peru ushindi.

Mechi hizi za nusu fainali zitachezwa tarehe 3 na 4 mtawalia mwezi huu. Huku fainali ikichezwa tarehe 7 mwezi julai.